Posts

KUNA GHARAMA YA KULIPA ILI UTEMBEE NA MUNGU

 KUNA GHARAMA YA KULIPA ILI UTEMBEE NA MUNGU 🔹Watu wengi sana wanapenda kutembea na Mungu katika maisha yao, na hicho ni kitu kizuri sana, lakini ni watu wachache sana ambao wanaelewa gharama wanayotakiwa kulipa ili wafanikiwe katika jambo hilo. 🔸Mungu anapenda kuona watu wake wanatembea pamoja nae kama walivyofanya wakina Henoko, Ibrahimu, Daudi n.k, lakini ana kanuni zake ambazo watu wake wanatakiwa kutembea nazo kila wakati. 🔹Kanuni kubwa ni kufanya mapenzi ya yake (yaani mapenzi ya Mungu) katika maisha yako. Yohana 8:28-29. 28. Basi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo.  29. Naye aliyenipeleka yu pamoja nami, hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo.  🔹Unapotaka kufanya mapenzi ya Mungu na kutembea pamoja nae katika maisha yako, unatakiwa kufahamu na kuzingatia mambo yafuatayo; 1. LA...

MAARAFA NI NINI?

 Watu wengi wanasema unaangamia kwa kukosa maarifa lakini hawajui maana ya maarifa nini. Maarifa ni nini? Maarifa ni njia inayotumiwa kujitoa katika shida. Maarifa ni njia ya kupata kitu. Maarifa ni Elimu au ujuzi.  Biblia inazungumza hapo juu kwamba watu wengi wanaangamizwa kwa kukosa maarifa, maarifa yanayozungumzwa hapa ni elimu na ujuzi sahihi wa Neno la MUNGU. Maana ya kwanza ya maarifa ni njia inayotumiwa kujitoa katika shida. Shetani ameleta shida nyingi sana na vifungo vingi sana kupitia mawakala zake wachawi, waganga na mizimu na watu wengi sana wameangamia kwa sababu tu wamekosa maarifa ya kuwatoa katika shida hizo. Biblia inajulisha ikisema kwamba Kumcha MUNGU ndio chanzo cha maarifa sahihi yanayoweza kumsaidia mtu ili atoke katika shida mbalimbali za kiroho, Hiyo iko Mithali 1:7 '' Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.'' Biblia inasema Ni wajinga peke yao ndio wanaoweza wakadharau Neno la MUNGU la kuwapa maarifa sahihi ...

Upendo wa MUNGU

 YESU NDIO NURU YA KWELI

KILA KONA IMEKUWA ((COVID-19

Image
DUH KILA KONA IMEKUWA ((Covid-19 Corona virus)) tambua Kabla ya corona kifo kilikuwepo na baada ya corona pia kifo kitakuwepo, Jitathimini ulipotoka, ulipo na unakokwenda.  2Wathesalonike 3:3 Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu. Utafanywa imara utalindwa na mwovu kwa shalti moja tu la kumpa YESU maisha yako nje ya YESU hakuna usalama aise!!!  Ndugu yangu mpendwa hivi ni kweli hivi ndivyo ulivyo? Ziko wapi nguo zako na viatu vyako vizuli? Iko Wapi gari yako V.X V.8🚗 uliyotamba nayo ukawamwagia watu maji Barabarani? Kwanini haupo kwenye nyumba yako nzuli ya thamani? Ngoja kwanza!! ziko wapi zile sherehe ulizokuwa ukizifanya na kusherekea kila kuchwapo? Iko wapi Digrii yako na Masters? Iko wapi passport yako na Visa? Mbona hauna hata ile ATM card 🏧 yako? Ooooh nini kimetokea kwenye meno yako na dimpozi zako? Iko wapi ile iPhone uliyoipenda Sana? Ziko wapi kumbukumbu zako za bank 🏦 (Bank statement)? Hivi nini kimetokea ...

AINA ZA HASIRA ZA WANAWAKE NA HEKIMA YA MKE KWA MUMEWE.

Image
AINA ZA HASIRA ZA WANAWAKE NA HEKIMA YA MKE KWA MUMEWE. 1. Kuna mwanamke ambaye akikasirika, huishia kulia tuu! 2. Lakini mwingine akichukia, anaongea saanaa muda wote hadi ikukere! 3. Mwanamke mwingine akikasirika, ananuna, haongei! Mtapishana tu kimya kimya. Mawasiliano kibubu-bubu. Shavu limejaa kama Kobra! 4. Mwingine akishikwa na hasira, period ya ghafla ghafla inafuata! 5. Wako wanawake ambao, akichukia, Atakachokishika usipokimbia anakutandika na anaweza kukuchoma na kisu,, majuto baadaye! 6. Mwanamke mwingine akikasirika, hasira zake zinaishia kwenye kuvunja-vunja vyombo. Au saa nyingine kugombeza- gombeza wafanyakazi na watoto! Dizaini hii, huwa ni wale waliokosa kukidhiwa haja za kihisia/ ndoa na waume zao! 7. Mwanamke mwingine akikasirika, Mtajuana kitandani panapo usiku, Nakwambia utaungama yoote! 8. Kuna wengine wakitibuliwa, hukimbilia kufunga mabegi na kuondoka! 9. Wapo ambao wakikasirika, wanagoma kupika! 10. Wengine wakichukia, wanaam...

KAMA GIDIONI

Image
1. Kama Gideon,  baadhi yetu tumefichwa na matatizo ambayo sisi ndio tunapaswa kuyatatua.  Tunazikimbia changamoto ambazo tuliumbwa ili tuzitatue. Toka Huko Mafichoni Aisee! 2. Wewe usipodhihirika, wengi wataathirika. Wito wa Mungu kwako ni muhimu sana, Hupaswi kuupuuzia. Viumbe vyote vinakusubiria udhihirike, tambua hilo, na Chukua hatua. 3. Weka woga kando, weka hofu kando, katika nchi yako ya ahadi lazima kuna majitu, lakini hayataweza kukudhuru. Wewe na Mungu ni jeshi kubwa, nenda kwa imani, nawe utaangusha milki za wafalme, na kuimiliki nchi yako ya ahadi. 4. Usikubali kukata tamaa. Usikubali kurudi nyuma. Usikubali kuvunjika moyo. Labda kwa wanadamu haiwezekani, lakini si kwa Mungu; ukiwa na Mungu, yote yanawezekana. 5. Wakati mwingine tunapitia mambo yanayotuumiza katika maisha, lakini mambo hayo hayo ndiyo yanaweza kuwa yanatuonesha kusudi na wito wa Mungu kwetu. Jiulize, mapito haya yatanifaa wapi? KUSUDI LAZIMA LITIMIE! Makubimsafiri@g...

UJUE UMUHIMU WA KUIOMBEA NAFSI YAKO

Image
UJUE UMUHIMU WA KUOMBEA NAFSI YAKO. Zaburi:42.2-6 Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai, Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu? Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako. Nayakumbuka hayo nikiweka wazi nafsi yangu ndani yangu, Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza nyumbani kwa Mungu, Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu. Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu. Nafsi yangu imeinama ndani yangu, kwa hiyo nitakukumbuka, Toka nchi ya Yordani, na Mahermoni, na toka kilima cha Mizari. Bwana Yesu asifiwe sana sana. Biblia inatueleza kuwa Nafsi ni uhai; kwenye; Mwanzo:2.7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. Na ukisoma kwenye 42:2 utaona neno likisema hivi;  "Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU,Mungu a...

COME HOME

Image
Today's devotion COME HOME John 3:16 " For God so loved the world that He gave His begotten Son that whosoever believes in Him should not perish but have everlasting life." Brethren in Christ, Jesus' death on the cross for our sins proves better than anything else that God loves mankind and desires to be with Him. Those of us who truly receive God and His word are His children and God wants His children to be near Him, both in this life and throughout eternity. In Luke 15 we learn of the story of the prodigal son on how he got his wealth from the father, how he squandered it and how he returned when he fell onto hard times. We see here that he returned with the spirit of a humble servant.  A child of God has not truly come home until he approaches the Father with a humble spirit. Are you child of God? If not, why not come home today? He is there waiting for you with open arms. May God bless you and have a wonderful day.

USIFADHAIKE MOYONI MWAKO

Image
USIFADHAIKE MOYONI MWAKO; Hata Kama Kuna Mapito Magumu Maishani Mwako Hata Kama Huoni Mlango Wa Kutokea Hata Kama Huoni Faida Ktk Kazi Yako unayofanya Hata Kama Unaona Maadui Wanazidi Kuwa Wengi Maishani mwako Hata Kama Hauupata Mkate Wa Kila Siku Hata Kama Kuna Udhaifu Ktk Mwili wako Hata Kama Kuna Changamoto Ktk Familia yako, Kumbuka Yesu Kristo Alisema Yote Yamekwisha kwa Kupigwa Kwake Sisi Tumepona Ametupumzisha Mizigo Yetu katika Kila Jambo Tunashinda Na Zaidi Ya Kushinda Ktk Yeye Aliyetupenda upeo ktk Kila Jambo Tulitendalo Tutafanikiwa na kushinda.  JIPE MOYO MPENDWA WANGU SAFARI BADO INASONGA NAWE U-MSHINDI. By Mt D. Makubi

INAWEZEKANA KABISA MWANAUME KUWA NA MWANAMKE MMOJA

Image
INAWEZEKANA KABISA MWANAUME KUWA NA MWANAMKE MMOJA Yaani sisi ni tai, ila hatuelewi, tunajifahamu kama kuku. Kwamba tunao uwezo mkubwa wa kuwa mwanaume wa mwanamke mmoja lakini tumeaminishwa kinyume chake tumeamini na tunaishi ndani ya uongo huo uliopikwa vizuri. Mkulima mmoja aliokota yai la ndege tai akalichukua na kwenda kulichanganya na mayai ya kuku wake aliyekuwa anatamia. Baada ya muda kuku akatotoa pamoja na lile yai la tai. Mama ambae ni kuku akamlea tai akijua ni mtoto wake, Tai akakua pamoja na vifaranga vya kuku, Akachakura jalala moja akitafuta chakula kama vifaranga wengine, Akienda huku, ‘kampani’ yake ilikuwa ni kuku, akirudi huku ‘kampani’ yake ilikuwa ni kuku. Siku moja, akiwa na kuku wengine akaona familia ya tai inapaa angani. Akatamani kuwa mmoja wa wale tai, kuwa kule juu, mawinguni akamgeukia kuku mmoja aliyekuwa karibu yake, akamwambia. “Natamani ningekuwa tai.” “Haitawezekana.” Kuku akamjibu, kisha akaongeza. “Wewe umeumbwa kuku, na utabaki kuwa ku...

USIPOBARIKIWA MJINI UTABARIKIWA MASHAMBANI

Image
USIPOBARIKIWA MJINI UTABARIKIWA MASHAMBANI Jina la Bwana wetu YESU KRISTO litukuzwe mpendwa wangu Karibu tujifunze Neno la MUNGU, Natamani somo hili liwafikie watu wengi zaidi wasome somo hili kuanzia mwanzo hadi mwisho, maana kuna kitu chake cha pekee ROHO MTAKATIFU amemuandalia kila mtu kupitia somo hili la ufunuo wa Mungu mwenyewe. Usipopata baraka mjini hamia mashambani utabarikiwa iko kwenye Biblia hii, Inawezekana likawa Neno gumu sana kwako ila nisikilize itakusaidia ili utoke na kitu usibaki kama ulivyo fungua akili yako kupokea kitu kipya. Kumbukumbu la torati 28:3  Utabarikiwa mjini, tabarikiwa na mashambani. Maana yake MUNGU anaweza kuachilia baraka popote iwe ni mjini au vijijini kwenye mashamba, Maana yake ukiona jambo moja limeshindikana kukuletea baraka unayo itarajia sio dhambi kuhamia jambo lingine. mfano kama biashara yako haikulipi hamia kwenye Kilimo, Kama kilimo hakikulipi hamia ufugaji, Kama ajira haikulipi basi jiajiri mwenyewe, baraka za MUNGU...

USHUHUDA WA ALIEKUWA WAKALA WA SHETANI

Image
USHUHUDA WA ALIYEKUWA WAKALA WA SHETANI. (Umetafsiriwa) Wapendwa rafiki zangu, napenda kuwashirikisha ushuhuda huu wa binti kutoka South Africa alyekuwa wakala wa shetani, alkuwa mtumishi wa shetani kwa miaka kumi na miwili na alpandishwa cheo akiwa huko. Nawasalimu kwa jina la Yesu Kristo, jina langu ni NONKOLISO NGELEKA kutoka Nzimakwe, nmefanya kazi mahali pale kwa miaka 12, nimezalia mwaka 1988, Nilifanya kazi mahali pale tangia nikiwa bint mdogo kadiri muda unavyoenda nikazidi kupanda daraja, kuna madaraja tofauti, kuna waabudu shetani makanisani bila kujua kama wanamwakilisha shetani, na wapo waabudu shetani ambao wanaweza kujitenganisha na miili yao yakawaida na kuwa kwenye ulimwengu wa roho (kama wachawi wanavyofanya), mimi nilkuwa kwenye kundi la pili la wanaojitenganisha n miili yao. Nilianza kuwa napata ndoto nikilala naota napigana kama ilivyo kwenye michezo ya kuigiza kwenye televisheni wakiigiza wanapigana maeneo ya mjini halafu kama wanapaa juu, baada ya sik...

HADITHI YA MDADA KIPOFU

Image
HADITHI YA MDADA KIPOFU Hapo zamani kulikuwa na Mwanamke kipofu ,alie chukia sana hali yake ya kuwa kipofu, alimchukia kila mtu kwakweli ikiwemo nduguze na wazazi wake isipokuwa Mchumba wake, alie mpenda na kumjali nakuwa nae wakati washida na raha hivyo alimthamini, alilia kilasiku na kujisemea kuwa SIKU ikitokea akaona Basi jambo la kwanza lingekuwa ni KUFUNGA NDOA na Mchumba wake huyo aliempenda sana na kumfanya kila kitu ktk maisha yake.... (kumbuka hii ni hadithi) Siku Moja alipata Bahati ya KUKOPESHWA Macho, ambapo aliweza kuona kila kitu kilicho kuwa mbele yake, Pamoja na Boyfriend Wake nae Boyfriend wake aliitunza ahadi ya mchumba wake sasa baada yakuwa sasa anaona alimuomba kama itawezekana sasa WAOANE Kama Alivyo AHIDI. Mdada huyo alishitushwa na hali aliyokua nayo Mchumba wake huyo maana Nayeye kumbe alikua KIPOFU pia kama alivyo kuwa yeye hapo kabla, mdada huyo alikataa KUOLEWA na Kijana kipofu aliejitoa na kuthamini kama nafsi yake, Boyfriend wake aliondoka huku M...

TOFAUTI KATI YA WATU WALIOFANIKIWA NA WASIOFANIKIWA

Image
Mafanikio ni aina ya tabia fulani ambayo mtu huijenga na haiji tu kwa bahati mbaya bali ni mpango mkakati unaopaswa kuwa nao maishani tofauti na hivyo you can kiss goodbye mafanikio leo tutaangalia hasa vitu vikuu vitatu vilivyobeba watu wanaofanikiwa na wasio fanikiwa. Wote tunakuja duniani baada ya kuwa washindi katika mapambano makubwa yanayohusisha mamilioni kwa mabilioni ya washiriki Wote tunakaa mapumzikoni miezi tisa tukijaandaa na pambano lingine, Wote tunakuja duniani tukiwa full packed na vitu muhimu vya kutusaidia kushinda mapambano mengine ya hapa duniani, ambapo Mungu humpa kila mtu vitu sahihi anavovihitaji kuendana na aina ya pambano lake, Yaani tunapewa vitu kama vile Passion, talents, core abilities, potential, akili, nguvu, viungo kutokana na kuendana na aina ya mapambano unayoyaendea, SWALI NI JE, NINI KINASABABISHA WENGINE WASHINDE MAPAMBANO YA HAPA DUNIANI NA WENGINE WASHINDWE ILI HALI WE ARE ALL WINNERS?? (Sisi wote ni washindi) Utofauti huanza kuonekan...

BWANA YU PAMOJA NAWE EE SHUJAA

Image
BWANA YU PAMOJA NAWE EE SHUJAA Waamuzi 6:12-16 12-Malaika wa BWANA akamtokea, akamwambia, BWANA yu pamoja nawe, Ee shujaa. 13-Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye BWANA, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani. 14-BWANA akamtazama, akasema, Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma? 15-Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu. 16-BWANA akamwambia, Hakika nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kama mtu mmoja. Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu, ninatamani sana uyajue mapenzi ya Mungu na Kusudi kuu la wewe kuwapo hapa duniani maana haupo duniani kwa bahati mbaya. Huwa namfurahia Mungu sana na nguvu zake n...