AINA ZA HASIRA ZA WANAWAKE NA HEKIMA YA MKE KWA MUMEWE.

AINA ZA HASIRA ZA WANAWAKE NA HEKIMA YA MKE KWA MUMEWE.


1. Kuna mwanamke ambaye akikasirika,
huishia kulia tuu!
2. Lakini mwingine akichukia, anaongea
saanaa muda wote hadi ikukere!
3. Mwanamke mwingine akikasirika,
ananuna, haongei! Mtapishana tu kimya
kimya. Mawasiliano kibubu-bubu. Shavu
limejaa kama Kobra!

4. Mwingine akishikwa na hasira, period ya
ghafla ghafla inafuata!
5. Wako wanawake ambao, akichukia,
Atakachokishika usipokimbia anakutandika
na anaweza kukuchoma na kisu,, majuto
baadaye!
6. Mwanamke mwingine akikasirika, hasira
zake zinaishia kwenye kuvunja-vunja
vyombo. Au saa nyingine kugombeza-
gombeza wafanyakazi na watoto! Dizaini hii,
huwa ni wale waliokosa kukidhiwa haja za
kihisia/ ndoa na waume zao!

7. Mwanamke mwingine akikasirika,
Mtajuana kitandani panapo usiku,
Nakwambia utaungama yoote!
8. Kuna wengine wakitibuliwa, hukimbilia
kufunga mabegi na kuondoka!
9. Wapo ambao wakikasirika, wanagoma
kupika!

10. Wengine wakichukia, wanaamua
kwenda kulala kimyaaa!!
11. Wanawake wengine wakikasirika,
tumbo linakata, na pengine mpaka
wanaharisha!

13. Wako ambao wakishikwa na hasira,
huingia kwenye maombi na kuugua
kusikoweza kutamkwa. Uchungu ukiisha,
wananawa uso na kwenda sokoni.
14. Yuko ambaye akishikwa na hasira,
hucheka saaanaaa.... Hutajua kama
amekasirika! Dizaini hii ni hatari sana,
maana anaweza kukudhuru kiurahisi.

HAYA DADA ZANGU HASIRA YAKO NAMBA
NGAPI?


Nyingine;
15. Mwingine akikasirika anafanya kazi kwa bidii kubwa. Hata kama nguo Safi anazifua tena

16. Mwingine akikasirika anaimba siku nzima.


17. Mwingine akikasirika anakimbia umbari mrefu.

18. Mwingine akikasirika anapigana na ukuta au anang'oa mti.

19. Mwingine akikasirika anajinyonga πŸ™†‍♂

20. Mwingine akikasirika anamchukia KILA mtu.

21. Mwingine akikasirika anakataa kula; anafunga kwa dharula

22. Mwingine akikasirika anakula sana.😁3in1

N.k

Hizi ni kwa wote

HEKIMA YA MKE KWA MUMEWE

Hakuna mwanaume mkorofi kwa mwanamke mnyenyekevu hata ungekuwa umemkosea nini...

Mwanamke ukijishusha na ukanyenyekea analainika tu...labda awe ana mapepo ndio unyenyekevu wako hautagusa moyo wake...

Mume hafokewi, mume hagombezwi, mume hafanyiwi jeuri na kiburi, eti akinuna na wewe unanuna, asipokutafuta na wewe humtafuti... UTAPOTEZA NDOA YAKO...

Huyo ni mume wako wa ndoa unaruhusiwa kumng'ang'ania kama "Ruba"...asipokutafuta mtafute, asipoongea na wewe ongea naye wewe...yakupasa kutambua hakunaga mke anayeambiwaga anajipendekeza kwa mumewe...

Kunyenyekea hakukugeuzi kuwa mtumwa au kupoteza nafasi ya kuwa mke bali kiburi na jeuri na hali ya ushindani ndio vitakufukuza kwenye hicho kiti na hiyo nafasi ya kuwa mke kwa haraka sana...

Elewa unatakiwa kuwa mnyenyekevu na sio kuwa Mpumbavu...panapotakiwa hekima na akili zitumike pia

❤️🏠NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE  NA MALAZI YAWE SAFI  MAANA WAASHERATI NA WAZINZI MUNGU ATAWAHUKUMIA ADHABU (WAEBRANIA 13: 4)


Makubimsafiri@gmail.com
Call +255756717689

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA YA NAFSI, ROHO, MOYO NA MWILI.?

USHUHUDA WA ALIEKUWA WAKALA WA SHETANI

BWANA YU PAMOJA NAWE EE SHUJAA