BWANA YU PAMOJA NAWE EE SHUJAA
BWANA YU PAMOJA NAWE EE SHUJAA
Waamuzi 6:12-16
12-Malaika wa BWANA akamtokea, akamwambia, BWANA yu pamoja nawe, Ee shujaa.
13-Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye BWANA, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.
14-BWANA akamtazama, akasema, Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma?
15-Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu.
16-BWANA akamwambia, Hakika nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kama mtu mmoja.
Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu, ninatamani sana uyajue mapenzi ya Mungu na Kusudi kuu la wewe kuwapo hapa duniani maana haupo duniani kwa bahati mbaya.
Huwa namfurahia Mungu sana na nguvu zake na uweza wake katika utendaji wake, huwa nikiangalia anavyofungua watu na kuwaweka huru anawapiga maadui na kurejesha furaha iliyopotea,
Mwana wa Mungu kuna ujumbe wako hapa kutoka katika tafakari ya Gidion, Gidion alijiona yeye hafai, alijiona dhaifu, mtu asieweza kuwaokoa wana wa Israel kwa mkono wa Mungu,
Gidion aliuliza maswali mengi lakini yote hii ni katika kupata uhakika wa Mungu wa kweli anaeishi, akitazama wazazi wake walikua wakiabudu miungu sasa akawa yuko njia panda, lakini Mungu huwa anachagua vidhaifu nakuvifanya kuwa vyenye nguvu na uwezo wa kubadilisha na kuthibitisha Jinsi MUNGU alivyo,
Tuone Bwana alichomwambia Gidion na namna ambavyo Gidion alichukua hatua za ujasili.
1. "Bwana yu pamoja nawe ee shujaa"
Tunaona kuwa Mungu anampa uhakika wa kuwa nae katika mambo yote yaani Mungu anajidhihilisha mwenyewe kwake, lakini Gidion hakujua kama tangu mwanzo alikua chini ya uongozi wa Mungu,
Mungu anapotaka kukutumia huwa anakupa uhakika kabla ya vyote au chochote, na kila alie okoka anauhakika wa kuongozwa na Mungu maana alisema katika Mathayo 27:19-20 Tazama Mimi nipo pamoja nanyi hata ukamilifu wa dahari wewe au sisi tuliompokea KRISTO kuwa BWANA na MWOKOZI wa maisha yetu.
Maana yake tunapaswa kutembea kifua mbele kila saa kila dakika, mahali popote tunapokuwepo Mungu yupo kujidhihilisha hivyo tumia hiyo nafasi kumdhihilisha Mungu anae ishi na kumiliki na kutawala kwakuwa yeye ni mtawala siku zote.
Nimekua nikirudia usijione dhaifu, katika udogo wako huo Mungu anakuamini katika udogo huo huo na anakutumia kwaviwango anavyotaka, kaa katika nafasi ya kutumika ili Mungu akutumia ipasavyo.
Ukiaminiwa aminika, na anaekuamini mwenyewe ni Mungu ooh hallelujah ni Neema iliyoje kutembea ukiwa umeiniwa na Mungu, tembea kifua mbele, halibu kazi za adui, ukiwa ofisini kwako, kwenye biashara zako kuna watu wanakuchezea tafuta sehemu ya Siri piga kinachosababisha udharaulike piga madhabahu wanazotegemea kisha jitamkie nakua juu katika jina la Yesu,
Ngoja nikwambie kitu mpendwa msafiri mwenzangu maisha ni vile wewe unataka kuwa ishi maisha ya kujitamkia Gidion japo alikuwa anamkanganyiko kichwani mwake lakini babo aliamini katika Mungu na aliishi maisha ya ushujaa na ingawaje alikuwa katika changamoto kadhaa.
2. "Enenda kwa uwezo wako huu"
Mungu hakumuangalia Gidion kama mtu dhaifu bali alimuona kama ni mtu mwenye nguvu na uwezo wa kukabiliana na na challenge zilizopo, kumbuka habari ya wale wakoma wanne walipokwenda kwenye kambi ya washami ambapo Mungu aliwasikilizisha washami hatua za wakoma kama jeshi kubwa la Israel, maana yake kuna nguvu aliiachilia kwa wale wakoma, na ile nguvu ndio alio iachilia kwa Gidion ndipo malaika anapomwambia Gidion Enenda kwa uwezo wako huu, kuna uwezo mpya aliuachilia ndani ya Gidion pasipo yete kujua kama ambavyo alifanya kwa wale wakoma wanne walioamua kuwa bora wakauwawe na majeshi ya washami Mungu aliachilia ujasiri ndani yao ndivyo ilivyokuwa kwa Gidion.
Ndio maana hata nawe kuna uwezo au nguvu ambayo Mungu ameiachilia ndani yako na ndio maana kuna wakati kuna picha inakuja ndani yako kuwa wewe ni mtu mkubwa, unakanisa kubwa kama wewe mtumishi, tajiri mkubwa, au ofisa mkuu katika kazi unayoifanya, hiyo ni hali halisi kwakua ndani yako kuna uwezo wa kipekee umewekwa lakini wewe hujui na ndio maana unaishi chini ya kiwango cha Ki-Mungu. Badilika sasa ishi kama mfalme, amuru viwe na kwa iman vitakuwa katika jina la Yesu.
3. "Nawe utawapiga wamidian kama mtu mmoja"
Nahisi kufurahi kwakua na huu uhakika aliopewa Gidion hata wewe Leo hii unao uhakika huu ambao Gidion alihakikishiwa, kwakua Yesu alikufa msalabani na kuachilia umiliki wako nakukupa nguvu kupitia damu ya yake pale msalabani.
Haijalishi mtaani kwako kuna wasumbufu kiasi gani, iwe wachawi, waganga, washirikina lakini kumbuka unaweza kuwapiga kama mtu mmoja, tazama sasa Mungu alichokifanya akamtumia Gidion Kuvunja madhabahu ya muungu baali!! Maana yake wewe pia unauwezo wa Kuvunja kila madhabahu na nguvu za adui na muovu ibilisi, wachawi ambao wamekuwa wakitawala mtaani kwako.
Simama sasa tubu kisha ingia kuvunja madhabahu na sanamu zao kisha utaona mpenyo mkubwa katika kila ufanyavyo, vunja ofisini kwako, vunja kwenye eneo lako la biashara vunja shulen na chuon unakosama utaona Bwana atakavyokufurahia na kukutumia katika utumishi wake.
Kumbuka pale ulipo mpokea YESU kuwa BWANA na MWOKOZI wako uliingia agano na kuunganishwa na MADHABAHU na KI-MUNGU.
Wewe nishujaa unaejidharau, acha kujidharau simama kishujaa ili Mungu adhihilike (ajidhihirishe) kwenye maisha yako na utumishi wako.
Nakutakia Baraka za Bwana Yesu ziwe juu yako katika kila hatua yako.
Kama umebarikiwa na ujumbe huu share kwa ndugu jamaa na rafiki zako popote pale facebook na kwenye magroup ya Whatsup hutaachwa hivyo hivyo bali utabarikiwa kwa kuitangaza injili kwa kushare. Pia like Facebook Page mwinjilist e Daudi Makubi kwa masomo mengi zaidi.
Ukipenda kutumiwa masomo ya Neno la Mungu kila siku kwa Whatsup tuma majina yako mawili inbox, whatsup kwa namba ya voda +255756717689
kuomba kuunganishwa kupewa masomo kila siku na utatumiwa, pia kwa ushauri na maombi piga namba hii hii, na Mungu wambinguni akubariki sana.
Facebook Mt D Makubi
Twitter Mt Daudi Makubi
Page yetu evangelist e Daudi Makubi
Instagram Mt Daudi Makubi
Email address makubimsafiri@gmail.com

Lucky Club Casino site - luckyclub.live
ReplyDeleteLucky Club Casino has over 40 exciting slots games that pay anywhere and anytime you want to deposit, we have it. It offers the latest in slots, table games luckyclub