NAMNA YA KUFUTA MANENO MABAYA ULIYO NENEWA KWA MAOMBI
Ujumbe huu ni wa maombi ili ufunguliwe nikuombe uombe sala hii ndugu kwa IMANI baada ya kuzaliwa upya, kuokoka au wewe ambaye tayari uko kwenye wokovu na umeshafanyika mtoto wa MUNGU kupitia YESU KRISTO, futa kila neno baya ambalo ulinenewa na wanadamu wazazi na hata majini.
Huu ni ufunuo ambao MUNGU alinipa kwamba kuna watu hata hawajafungwa na mapepo ila wamefungwa na maneno ya watu tu na ikumbukwe kuwa kinywa kinaumba kuna watu Hawaolewi au kuoa kwa sababu tu ya maneno waliyonenewa ambayo yamewakamata hata leo, kuna watu hawaendelei kwa sababu walinenewa umasikini Nk.
Maombi ni njia yako ya kutoka kwenye vifungo vyote.
Mathayo 7:7-8 " Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa."
Omba maombi haya kwa imani.
''Kwa Jina La YESU KRISTO. Nayafuta Maneno Yote Mabaya Ambayo Wanadamu Wameninenea, Nayafuta Kwa Damu Ya YESU KRISTO Maneno Mabaya Aliyoyanena Yeyote juu yangu Awe Ni Mtumishi, Awe Ni Ndugu, Awe Ni Rafiki, Wawe Ni Wazazi Wangu Wa Kimwili Na Kiroho, Kama Ni Maneno Mabaya Na Yaliyo kinyume cha MUNGU BABA Nayafuta Kwa Damu Ya YESU KRISTO.
Kila Mpango Wa Kishetani Unaoletwa Kwangu Nauvunja Na Kuubomoa Na Kuuharibu Na Kuuangamiza Kwa Jina La YESU KRISTO Sawasawa Na Yeremia 1:10. Vikao Vyote Vya Wachawi Na Mashetani Vya Kunijadili Mimi nisifikie mpango wako Eeh BWANA Naviangamiza Kwa Moto Wa ROHO MTAKATIFU
Tena Jina La YESU KRISTO Ni Ngome Imara Na Sasa Nakimbilia Ili Nikae Salama Kama Mithali 18:10 Inavyosema, Naharibu Ukungu Wote Wa Kipepo Kwa Jina La YESU KRISTO Kila Kuhani Wa Kishetani Anayefanya Vita Na Mimi Au Ndugu Zangu Au Rafiki Zangu Namponda Kwa Nyundo Maana Neno La MUNGU Ni Nyundo, Wapondeke Sasa Kwa Jina La YESU KRISTO Mwamba Wa MUNGU alie hai,
Asante Sana BABA Wa Mbinguni Kwa Uzima Huu Mkuu, Katika Jina La YESU KRISTO Nimeomba na kuamini
Amen Amen.
Maombi yangu kwako ni haya kwa wewe uliyechukua tendo la imani na kuomba maombi hayo hapo juu kwa IMANI.
BWANA MUNGU Katika Jina La YESU KRISTO, Naungana na Maserafi, Makerubi, na wazee ishirini na nne wenye uhai Nakuabudu Na Ninakushukuru Kwa Kumlinda Rafiki Yangu Huyu katika CKRISTO,
BWANA Naomba Umlinde Tena Leo Na Siku Zote, Maadui Zake Waabike Wao, Wanaomuwazia Mabaya Yawapate Wao Kwa Jina La YESU KRISTO. Naziangamiza Kwa Jina La YESU KRISTO roho Zote Chafu Zilizotumwa Kwake, Naiteketeza roho Ya Magonjwa Kwa Jina La YESU KRISTO,
Hataugua Wala Kuuguza, Naiharibu roho Ya Madeni, Hatakopa Bali Atakopesha Kwa Jina La YESU KRISTO, Naiteketeza roho Ya Mauti Inayomfuatilia, roho Ya Mizimu, roho Ya Mateso Na Kuonewa, roho Ya Kukataliwa Na Kila roho Kutoka Kuzimu Kwa Jina La YESU KRISTO.
Kila Mchawi Anayepanga Uchawi Kwa Ajili Yake, Ninauharibu Uchawi Huo Kwa Jina La YESU KRISTO, Nawaponda Wachawi Wote Kwa Jina La YESU KRISTO, Kila Kafara Ya Damu Waliyotoa Watu Wabaya Kwa Waganga Wa Kienyeji Ili Damu Hiyo Iwe Inamlaani Ndugu Huyu Asifanikiwe Ninaifuta Damu Hiyo Kwa Damu Ya YESU KRISTO, Kwa Moto Wa ROHO MTAKATIFU Na Kwa Jina La YESU.
Asante BWANA.
Ni Katika Jina La YESU KRISTO Nimeomba.
Amen Amen.
Niishie hapo kwa Leo MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine, na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho ktk kanisa. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi nduguyo
Mt Daudi Makubi
Mobile, Telegram & whatsApp
+255756717689
Email makubimsafiri@gmail.com
Comments
Post a Comment