UPENDO HUTAMBUA NA KUHESHIMU WENGINE

Huku kwetu leo tuna neema ya mvua mvua kidogo, lkn nilipokuwa nikitafakari maneno ya Mungu asubuhi hii ktk kitabu Cha Rumi 12:9-10. Nikaona kitu muhimu cha kukushirikisha nacho ni :-
(UPENDO HUTAMBUA NA KUHESHIMU WENGINE)

"Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;"
Warumi 12:9-10

Kuna msemo huu nisiokumbuka ni wa nani "Before you preach the word know the world" yaani kabla ya kuhubiri neno ujue/utambue/ufahamu ulimwengu,
Na hii ni tabia ya upendo kutambua na kuheshimu wengine,

Hujaumbwa peke yako na wala wewe na mimi sio kisiwa bali tupo pamoja na watu mbalimbali wanaokubaliana na wasiokubaliana na tunachoamini. Wenye tabia tofauti na sisi, mitazamo tofauti iwe sahihi au isiwe sahihi,

Kuna wakati wanafunzi wa Yesu walikutana na watu wengine (wanafunzi) wakihubiri injili wanayohubiri na wakawakataza, Moja hawakuwatambua lakini mbili hawakuheshimu pamoja kwamba walihubiri injili ile ile (MARKO 9:38-39)

Changamoto kubwa katika kutambua ni kwamba cha kwanza yapaswa kujitambua wewe ni nani ndipo itakuwa rahisi kutambua wengine na kuwaheshimu.

Ni kweli una kipaji kimestawi sana lakini bado inabidi utambue na kuheshimu vipaji vya wengine na hiyo ni tabia ya upendo.

Ni rahisi sana mtu kumtendea wema mtu kwasababu hajui historia yake au tabia yake. Lakini akigundua kuwa anahistoria mbaya au tabia mbovu anaweza jilaumu Kwanini alimsaidia au kumtendea wema.

Upendo unatambua na kuheshimu na unatenda wema sio kwasababu unayemtendea wema ni mtenda mema au mtenda mabaya bali kwasababu ni mtu.
Kutotambua wengine kunaweza kukufanya ujihesabie haki.

Kutotambua uwepo wa wengine kwenye maisha yako kunaweza kukufanya uanze kujisikia na kujivuna.

Kutotambua kwamba unaishi kwa ajili ya wengine itakufanya usiweze kuonyesha upendo ule unaopaswa kuwapa hao wengine. Na kutotambua kunaweza sababisha usiheshimu wengine pia. Kuheshimu wengine haina maana kwamba unakubaliana na kila kitu kwao.

Kuheshimu wengine haina maana kufanya vile wanafanya wengine. Ila ni kutambua na kujua wao nao ni watu na wanahitaji upendo na kusikilizwa pia na wanamchango katika maisha yetu iwe moja kwa moja au laa.

Mungu hakutupenda kwasababu hakutambua kwamba tu wenye dhambi. Pamoja na kwamba alitambua tu wenye dhambi bado alitupenda hivyo hivyo. Na akaja kutuokoa ila cha ajabu na kushangaza hamlazimishi mtu bali anaheshimu maamuzi ya kila mtu bali ameshatuonyesha matokeo ya maamuzi yetu, Hii ni kwasababu upendo unatambua na kuheshimu Wengine.

Wako shambani mwa BWANA
Mt Daudi Makubi Singida Maduka saba Church
WhatsApp:-+255756717689
Email:-makubimsafiri@gmail.com
MUNGU AKUBARIKI.

Comments

  1. Mungu hakutupenda kwasababu hakutambua kwamba tu wenye dhambi. Pamoja na kwamba alitambua tu wenye dhambi bado alitupenda hivyo hivyo. Na akaja kutuokoa ila cha ajabu na kushangaza hamlazimishi mtu bali anaheshimu maamuzi ya kila mtu bali ameshatuonyesha matokeo ya maamuzi yetu, Hii ni kwasababu upendo unatambua na kuheshimu Wengine.

    ReplyDelete
  2. Kweli upendo ni nguzo kuu ktk Maisha ya wanadamu wote lkn tunajisahau Na kukaa mbali kana kwamba hatujui asili yetu, as tunatokana Na Mungu Na Mungu ni pendo asante sana hkk nabarikiwa mtumishi Na mafundisho haya.

    ReplyDelete
  3. Amina Amina Utukufu una yeye Bwana YESU milele yote.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

NINI MAANA YA NAFSI, ROHO, MOYO NA MWILI.?

USHUHUDA WA ALIEKUWA WAKALA WA SHETANI

BWANA YU PAMOJA NAWE EE SHUJAA