HADITHI YA MDADA KIPOFU

HADITHI YA MDADA KIPOFU

Hapo zamani kulikuwa na Mwanamke kipofu ,alie chukia sana hali yake ya kuwa kipofu, alimchukia kila mtu kwakweli ikiwemo nduguze na wazazi wake isipokuwa Mchumba wake, alie mpenda na kumjali nakuwa nae wakati washida na raha hivyo alimthamini, alilia kilasiku na kujisemea kuwa SIKU ikitokea akaona Basi jambo la kwanza lingekuwa ni KUFUNGA NDOA na Mchumba wake huyo aliempenda sana na kumfanya kila kitu ktk maisha yake....

(kumbuka hii ni hadithi)
Siku Moja alipata Bahati ya KUKOPESHWA Macho, ambapo aliweza kuona kila kitu kilicho kuwa mbele yake, Pamoja na Boyfriend Wake nae Boyfriend wake aliitunza ahadi ya mchumba wake sasa baada yakuwa sasa anaona alimuomba kama itawezekana sasa WAOANE Kama Alivyo AHIDI.

Mdada huyo alishitushwa na hali aliyokua nayo Mchumba wake huyo maana Nayeye kumbe alikua KIPOFU pia kama alivyo kuwa yeye hapo kabla, mdada huyo alikataa KUOLEWA na Kijana kipofu aliejitoa na kuthamini kama nafsi yake, Boyfriend wake aliondoka huku MACHOZI yanamtoka kwa uchungu mwingi aliokuwanao.

Tunajifunza nini ktk hadithi hii Hivi ndivyo TABIA ya BINADAMU hubadilika pale ambapo STATUS zao ZINAPOBADILIKA, naomba ukubaliane na ukweli huu ni watu wachache Sana hukumbuka JINSI maisha yalivyo Kua hapo kabla hawajafakiwa, kina nani walikuwepo upande wao Kwa SHIDA na RAHA, hata wakati wa MAGONJWA....!


ISHI UKIKUMBUKA MAISHA NI ZAWADI

√KABLA hujawaza kumwambia MTU maneno MACHAFU/MABAYA
>Fikiria Mtu ambaye Hawezi/Hajawahi KUONGEA kabisa maishani mwake au amepitia magojwa na shida mbalimbali zilizompelekea kutokuongea.

√KABLA hujaanza KULALAMIKIA ladha ya CHAKULA
> Fikiria MTU amabae Hajapata MLO hata Mmoja TOKA asubuhi na hajui wapi pa kuupato mlo huo.

√KABLA Hujaanza kulalamika kuhusu MUME/MKE
> Fikiria MTU amabae ANAMLILIA MUNGU kila SIKU ampe Faraja na yaani ampatie ubavu wa maisha yake.

√KABLA hujaanza KULALAMIKA kuhusu Maisha
> Fikiria MTU ambaye AMEFARIKI/KUFA na KUIACHA DUNIA hii, lkn ww upo unaishi umempa nini MUNGU mpaka uwe hai mpaka leo.

√KABLA hujaanza KULALAMIKA kuhusu WATOTO wako
> Fikiria MTU ambaye anatamani apate WATOTO lakini ndio hivyo MUNGU hajamjalia anatamani kama kama angepata hata kama hao wako.

√KABLA hujaanza KULALAMIKA kuhusu Nyumba yako kuwa CHAFU,
>Kuna MTU hajasafisha Wala Kupalilia na kuiweka katika Hali SAFI
> Fikiria watu wanao LALA Mtaani Na Kwenye MITARO wakipitia hali ngumu na shida za kila namna.

√KABLA hujaanza KULALAMIKA kuhusu UMBALI unaoendesha GARI kwenda Popote HATA iwe kazini
> Fikiria Kuna MTU anatembea UBALI huo huo tena kwa MIGUU huko Kijijini na wengine ni maeneo hayo hayo unayoishi.

√KABLA hujaanza KULALAMIKA kuhusu Kazi yako
> Fikiria watu wasio na kazi, walemavu na wasiojiweza wanao Omba omba huko Mtaani na Kuwaza wapate wapi KAZI hata kama YAKO lkn sivyo ilivyo.

√KABLA hujaanza nyooshea watu vidole
> Kumbuka Kua hakuna Duniani asie na DHAMBI na WOTE tutahukumiwa na MUNGU MMOJA siku moja,
> Hivyo tunapaswa kutengeneza maisha yetu ya kesho maana hatujui ni lini MUMGU anakuja KUHUKUMU ulimwengu.

√Na ukiwa na Mawazo, mambo magumu, MAISHA, na Kadhalika yanayo kunyima FURAHA kila SIKU, TABASAMU na SHUKURU MUNGU wewe UPO HAI na BADO waendelea KUISHI.

Dada aliomba na kuweka ahadi siku akiweza kuona atafunga ndoa na kijana alie kuwa rafiki wa karibu sana ambaye alimchukulia kama nafsi yake angawa wazazi wa dada huyo na ndugu, jamaa walimuuza lkn kijana huyo alijitoa kwa dada, siku ikafika akaona vilivyzumguka na vilivyomo duniani akamkana yule kijan aliekuwa faraja yake siku zote, kumbe wakati mwingine mtu anaekuthamini huondoa nafasi yake kwa ajili yako anafanya kila jambo ili kuhakikisha una furaha pasipo kuangalia anagharimika kwa namna gani lkn tu uwe na furaha.

Ni vivyo hivyo YESU alikuja duniani kwa sababu ya upendo aliokuwa nao kwa wanadamu Yohana 3:16 Kwa maana Jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili kila mtu amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele.


Ni upendo ulimsukuma KRISTO hata akaicha ENZI ya MBINGUNI akaja kutukomboa kutoka  utumwani mwa dhambi ili tuwe huru, hakuwa na uhitaji bali aliuona uhitaji wetu wanadamu alijitoa ili kutuweka huru, kutufungua kutoka vifungo mbalimbali vya muovu ibilisi kama vile
•Ulevi
•Uesharati
•Uvutaji wa sigara
•Uongo
•Tamaa kutamani visivyo vyako
•Wizi
•Kusingizia
•Uchawi  N.K
YESU alikuja kutuweka huru ktk yote hayo na si hivyo tu bali kutupatia maisha ya umilele.

MAISHA NI ZAWADI TUISHI TUFURAHIE KILA SIKU KWA KUTHAMINIINA NA KUWASHUDIA WASIONJUA HABARI ZA KRISTO WAMJUE NA WAWEKWE HURU MAANA YESU NI WA WOTE.

LIKE & SHARE ili Kuwatia MOYO na wengine

No +255756717689
makubimsafiri@gmail.com
Facebook Mt D. Makubi
Twitter Mt Daudi Makubi
Instagram Mt Daudi Makubi.
Website mtdaudimakubi.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA YA NAFSI, ROHO, MOYO NA MWILI.?

USHUHUDA WA ALIEKUWA WAKALA WA SHETANI

BWANA YU PAMOJA NAWE EE SHUJAA