USHUHUDA WA ALIEKUWA WAKALA WA SHETANI



USHUHUDA WA ALIYEKUWA WAKALA WA SHETANI.

(Umetafsiriwa)
Wapendwa rafiki zangu, napenda kuwashirikisha ushuhuda huu wa binti kutoka South Africa alyekuwa wakala wa shetani, alkuwa mtumishi wa shetani kwa miaka kumi na miwili na alpandishwa cheo akiwa huko.

Nawasalimu kwa jina la Yesu Kristo, jina langu ni NONKOLISO NGELEKA kutoka Nzimakwe, nmefanya kazi mahali pale kwa miaka 12, nimezalia mwaka 1988,
Nilifanya kazi mahali pale tangia nikiwa bint mdogo kadiri muda unavyoenda nikazidi kupanda daraja, kuna madaraja tofauti, kuna waabudu shetani makanisani bila kujua kama wanamwakilisha shetani, na wapo waabudu shetani ambao wanaweza kujitenganisha na miili yao yakawaida na kuwa kwenye ulimwengu wa roho (kama wachawi wanavyofanya), mimi nilkuwa kwenye kundi la pili la wanaojitenganisha n miili yao.

Nilianza kuwa napata ndoto nikilala naota napigana kama ilivyo kwenye michezo ya kuigiza kwenye televisheni wakiigiza wanapigana maeneo ya mjini halafu kama wanapaa juu, baada ya siku tatu ndoto ikajirudia, nikasikia sauti ikiniuliza kama nataka kuwa vile nikajibu ndio akaniambia twende, tulipoondoka nilitenganishwa na mwili wangu na kuna shetani alibaki na mwili wangu na mm nikaenda kufanya kazi kuzimu. Nilipofika nikapewa namba (code) nikapewa na damu ya watu kwa sababu natakiwa kuishi kwa kunywa damu za watu kama chakula ili niweze kupoteza utu/ubinadamu nianze Kuwa na tabia kama za mnyama.

Kila daraja kuna namba inayowakilisha, namba 3 inawakilisha waabudu shetani namba 6 inawakilisha (Satanist), Satanist ni mtu ambaye alkufa akiwa mwabudu shetani, number 9 inamwakilisha Shetani mfalme wa mashetani, Lusiferi ambaye alfukuzwa mbinguni kwa sababu ya kiburi.


Nilfanya kazi mahali pale, mwanzoni nlkuwa kwenye kundi la kusababisha ajali barabarani ili majini waweze kupatĂ  damu ya akunywa na ili shetan (chifu) wa mahali pale aweze kupata damu ya kunywa. Kuna machifu wanaoongoza kwa kila eneo, kwa mfano Nzimakwe wana chifu wao ambaye ni Satanisti, kama nlvyoeleza hapo awali kuwa Satanisti ni nani, kama anahitaji damu tunatakiwa kusababisha ajali kwenye hilo eneo. Tunaposababisha hiyo ajali, tunaenda katika roho na hakuna mtu atakayeweza kutuona kwa macho na tunatupa pete mbele ya dereva na anaanza kupoteza umakini na gari linatoka nje ya barabara na watu wanakufa na chifu anapata damu.

Lakini sisi kama wafuasi wapya tulkuwa hatuwezi kuepuka kuishi bila kunywa damu, tulkuwa tunapewa damu hiyo kila mara. Machifu wanaishi zaidi kwenye mito, huwa wanakuja juu tu pale ambapo kuna kuwa na uamsho na matukio mengine ya kikanisa. Shetani anaishi baharini, sisi kama wafusi wapya tunaishi kwa damu ambayo tunachukuwa kwa binadamu wanaoishi, tunaweza tukasimama pemben ya mtu labda kwenye kituo cha mabasi au sehemu nyingine halafu tunaanza kumnyonya damu sana sana kwa watu ambao wana bidhaa zetu,
tulyemnyonya damu atajisikia kachoka na kama ana huzuni, na anaweza akadhani kwamba amekuwa tu na siku mbaya, lakini kumbe mara nyingi ni sababu waabudu shetani wamenyonya damu yake kwenye ulmwengu wa roho, lakin huwa hafi baada ya kufanyiwa hivyo.
Lakini kama wewe ni Mkristo ulyeokoka na unaishi maisha ya utakatifu hatuwezi kunyonya damu yako, kama tukijaribu kufanya hivyo roho wa Wakristo atawatetea na tutaungua kwa moto wake, hivyo hivyo kama tukisababisha ajali miongoni mwa abiria kukiwa na Mkristo alyeokoka hatutaweza kunywa damu ya wale watu waliokufa kwenye ajali kwa sababu damu yake inaharibu damu yote ilyoko kwenye ile benki yetu ya damu, na kama ikitokea tukanywa tinapoteza nguvu na kushindwa kufanya kazi zetu. Hata shetani na Machifu hawawezi kunywa damu hiyo.

Kama mtu anaishi maisha ya utakatifu na hatumii bidhaa zetu, kama bikini (G-string panties) ilkuwa ni kazi yangu kuzitambikia na kuzilaani (kuziwekea nguvu za giza), hereni, cheni, rangi za kucha, aina zote za nywele bandia iwe umebondi au Kusukana bidhaa zote za dhahabu ni za shetani.

Hivyo kama unatumia hiv vitu hata kama umeokoka kama tunataka kuja kukushambulia tutatumia namba yetu (code) kama umevaa hereni au unayo kabatini kwako, tutakuja na kukuta nyumba yako imezungukwa na ukuta wa moto kutoka kwa Mungu, na tuta-scan kwa namba yetu tutaingia, hivyo tukifika kwako tutaingiza namba kama ilivyo mtu anaingia stoo kwakwe kuchukuwa kitu fulani.

Hiyo ni kwa sababu, hereni na nywele bandia ulzonazo ndani zina code/namba yetu, na nitaitumia kuingia ndani na kufanya chochote ninachotaka kufanya na wewe, Huwa inatokea mtu anakuwa na utakatifu hata kama anatumia bidbaa zetu, lakini hatari yake ni kwamba mtu huyo awez kulindwa/kuwa na ulinzi.

Tunapokuja kwenye nyumba yako tukakuta umelindwa tunaenda kukuishtaki kwa Mungu kama mnavyojua shetani ndo mshtaki wa wanadamu, tunamwambia Mungu tunataka kuchukuwa product zetu, ikiwa ni hereni, nywele bandia wigi, rangi za kucha au bidhaa yoyote ya kwetu, tunaingia tunafanya chochote tunachotaka kufanya, kwa sababu tunajua Mungu ni mwaminifu na hawezi kuiba tuna ishtaki kwake na kumwambia inakuwaje anamfunika huyo mtu kwa ukuta wa moto wakati kunavitu vyetu anavyo ndani kwake? Hapo ndo inapoonekana hatari ya kutumia bidhaa za shetani mana unakosa ulizi , hivyo tunapofika ndani kwako tunachukuwa utakatifu wako kidogo kidogo, tunaenda kutambikia na kutamka laana kwenye zile bidhaa zetu (heren, lipstic, artificial hair) natunatamka kuwa atakaye vitumia ajae tamaa na laana iwe juu yake,.

Ikiwa ni mapambo ya dhahabu (jewellery) tunatanganza kuwa atakayezivaa awe kahaba na asiwe mtiifu (Ukahaba rohoni si lazima kuuza miili kwa ajili ya fedha ni kwenye tabia tu ya jinsi mtu anavyo vaa).

Nmefanya sana kazi kwenye vitu hivi, ikafika muda nikapandishwa cheo, kwa sababu nlfanikiwa sana kwenye kazi hii na nikaongezewa namba kwenye code yangu kwa sababu nilfaulu darasa la kuomba na kunenea laana kwenye nywele bandia, hereni mikufu na vitu kama hivyo

Nikapandishwa cheo kuanza kufanya kazi na makanisa, nilipokuwa kwenye kazi/daraja hili nilienda kwenye makanisa mengi ya wachungaji wanaofahamika, nikifika kwenye kusanyiko/event, mara nyingi kwenye makusanyiko ya uamsho nlkuwa nabeba pete tatu za mikononi/bangili, na mbili za vidoleni, bangili tatu nazirusha katikati ya kanisa na pete za vidoleni natupa mbele ya mchungaji, moja kulia na moja kushoto, kama mchungaji akiomba pete ya kwanza itakuwa inazunguma kanisani na nyingine itarudi kwangu, kama nlvyosema huwa naombea hizo pete tangu zikiwa zinatengenezwa nazinenea laana na tamaa juu yake, hapo Mchungaji atamuona masichana mrembo amekaa mbele yake na akianza tuu kupata mawazo ya tamaa juu yake hapo hapo anapoteza utakatifu (holliness) wake kwa sababu wote tunajua kwamba Roho Mtakatifu hakai mahali penye mawazo machafu, hivyo ndo jinsi tulvyokuwa tunawaangusha wachungaji.

Wakati mwingine Mchungaji anaweza akawa amesimama vizuri na pete zetu zisifanye kazi, hapo tunawatumia wake zao, kama mke wake anatumia bidhaa yetu yoyote tunazitumia kufanyia kazi usiku kama nilvyosema tunavyofanya kwa watu wengine wanaotumia hizo bidhaa

Hapo mke wa mchungaji ataanza kubadili mafundisho, kama walkuwa wanasema hereni na nywele bandia hazitakiwi ataanza kusema hakuna tatizo lolote kwa mtu akitumia hivyo vitu na mchungaji atakubaliana nae kwa sababu ni mke wake na ni mwili mmoja, nlfanya kazi sana na wachungaji na wengi nlfanikiwa kuwaangusha. Mchungaji alyekuwa anahubiri waumini wake wakae mbali na dhambi ataanza kuhibiri msichana anaruhusiwa kuwa na rafiki wa kiume mmoja, na mvulana awe na rafiki wa kike mmoja kabla ya ndoa, atabadilika na kuanza kusema ibada kwa wazee waliokufa zinaruhusiwa.

Ngoja nieleze kitu hapa, watu waliokufa sio mashetani na hawawezi kufanya kitu chochote hapa duniani tena kwa sababu wanasubiria siku yao ya hukumu, tunachofanya tunaenda makaburini na kuvaa sura zao na kuwatokea wale ndugu zake na sana sana tunawatokea wale walio na vipawa vya kiroho/waonaji na kuwaambia kuwa wanatakiwa kuwa waganga wakienyeji/sangoma

Anapo anza na hiyo tu, mtu huyo atatambulishwa kwa nyoka na nyoka anamwakilisha shetani mwenyewe. Wakati unafikiri ni mababu zako wanazungumza na wewe sio wao ni sisi,
Tunakuja kwenye nyumba tunapoitwa na harufu ya moshi wa matambiko na tutakunywa damu ya matambiko iliyotolewa kwetu bila wao kujua tutalala kwenye vitanda vyao na kufurahia.

Wakati mtu anakaribia kufa tunatumwa pale kuangalia kama mtu huyo anautakatifu wowote, kama hana tunaandika jina lake kwenye kitabu chetu siku ya hukumu ikifika wataenda kuchomwa pamoja na sisi, tunajua tutachomwa mwishoni mana tunaambiwa

Wakati mwingine tunaambiwa tufunge siku 40 hadi 60 kama kuna mchungaji ataenda kuhubir mahali kwa sababu hakuna kitu kinachoendelea duniani tusikione. Kama ikitokea nimefunga chini ya siku 40 napewa adhabu kwa sababu natakiwa kufika kwenye hilo eneo Mchungaji analohubir nikiwa na nguvu, nafika mwenye hilo eneo wa kwanza naanza kutamka laana ili watu wasisikilize mahubir na wasitubu na Chifu wa lile eneo asiungue na maombi yatakayoendelea pale, pia nashuka chini kwa ajili ya kwenda kumlinda asiungue kama akiungua utaona hadi walevi wameokoka wanasena Yesu Kristo ni Bwana, na ukiona vitu kama hivyo vimetokea ujue mchungaji alyekuwa anahubir aliomba na Chifu wa lile eneo kaungua na shetan kakimbia, mana kazi ya huyu shetani wa hapa ambaye ni Chifu ni kukaa katika makazi hayo na kuwazunguka watu na nguvu za giza na kuhakikisha hawaokoki na wale wanaokunywa pombe wasiache kunywa mpaka siku watakayokufa, na waliofungwa jela wafie humo, wanaoabudu sanamu na mizimu waendelee hadi watakapokufa, makahaba waendelee kufanya ukahaba mpaka watakapokufa.

Nlkuwa sifanyi kazi upande wa pwani ya kusini, kwa sababu ndo ninakotokea, nmefanya kazi sehemu nyingine kama Durban na maeneo mengine, nilipokuwa kuzimu walkuwa hawaniiti kwa jina langu bali kwa namba (code) nlyopewa, kwa mfano wanaweza wakaniita nifanye haraka kwenda Swaziland au Durban kuna kiwanda kimeshamaliza kutengeneza/kuzalisha hereni naenda pale kwa ajili ya kuzitambikia kabla hazijawekwa store ilkuwa ni kazi yangu kufanya hivyo.

Mwaka uliofuata nikatumwa kwenda Ntuzuma kulikuwa na Mchungaji kule, sitasema jina lake, nilitumwa kuchukuwa utakatifu wake, huyu mchungaji alkuwa kwel mtu wa Mungu alyeokolewa na ushuhuda wake ulkuwa unashangaza wengi, nlpofanikiwa kuchukuwa utakatifu wake nilipandishwa cheo, nikawa muhitimu/graduate sasa kazi yangu ilkiwa ni kuweka mitego kanisani, hakuna kitu ambacho nlkuwa siwezi kufanya, kuzimu tulkuwa tunatumia biblia pia hatufanyii kazi vitu ambavyo havijaandikwa kwenye biblia, kama biblia inavyosema mwanamke afunike kichwa akiwa kanisani tunaibadilisha na kusema sio lazima kufunika kichwa akiwa kanisani, na mwanamke anapokuwa hajafunika kichwa tinamshtaki kwa Mungu na kusema anakubalije kuwa yule ni mwanae wakati ameingia kanisani kichwa wazi? Tulkuwa tunabadilisha kilchoandikwa kwenye biblia, kwa mfano mwanamke hatakiwi kuvaa mavazi yampasayo mwanaume ndo mana huwa tunaweka laana/cham kwenye suruwali wanazovaa wanawake ili wazidi kuzivaa zaidi na zaidi ili wasimuone Mungu kwa sababu ya kutokutii kwao.

Baada ya kuhitimu/graduate kwangu sikuwa nafanya kazi moja kwa moja na kanisa tena, nlkuwa tu napita kutengeneza waabudu shetani naondoka, hawa wanakuwa hawajui kama wanamwabudu shetani lakini wanafanya pasipo kujua, kwa sababu hatuwatenganishi na miili yao kama mimi nilvyo, lakini tunawatumia kama wana bidhaa zetu kama nlvyoeleza hapo mwanzo, wataanza kuongea umbea kanisani, kila wakati wanalalamika, kuongea uongo kuhusu watu wengine, na kusema wachungaji wanachotaka ni hela tu, na vitu kama hivyo, watu wataanza kutokwenda kanisani kwa sababu ya hao waabudu shetan wasiojijua, baada ya hapo naondoka zangu nawaacha wakiendelea na kazi yao naenda kanisa lingine kuchukuwa ripoti halafu ntarudi baadae kuangalia uharibifu walioufanya kanisani,

Sasa watu hawa ambao tumewafanya waabudu shetani wanaanza kubadili mafundisho na kusema hakuna tatizo la suruali kwa wanawake, imani iko moyoni sio kwenye mavazi, hapo wanakuwa wanatusaidia kufanya kazi zetu bila wao kujua kwa sababu wanakuwa wanatuwakilisha, ukweli ni kwamba mwanamke hatakiwi kuvaa suruali, kwa hiyo wanaposema kuwa zinaruhusiwa na wanaposema watu waje tu na hereni kuabudu na kufanya shughuli za kanisa halafu watajifunza mbele ya safari au wakati Mchungaji anasema watu wenye mahusiano ya kimapenzi kabla ya ndoa/rafiki wa kike na kiume waje kwenye kwaya waongoze kusifu na kuwaombea watu basi huyu Mchungaji ni wakwetu na anafanya kazi kwa niaba yetu.

Ngoja nikwambie wakati wanasema wataacha dhambi, tutakuja kuwashinikiza kutokuachana na dhambi, wataendelea kufanya dhambi na tutasababisha iwe zaidi na zaidi, kwa mfano kama kuna msichana anauhusiano wa kimapenzi na mvulana tutasababisha hata yule mvulana aseme anataka kumuoa, na sio kwamba atafanya hivyo kwel hapana, tunataka waendelee na uhusiano huo ili waendelee kumkosea Mungu na waone hiyo dhambi ni kawaida mpaka kurudi kwa Yesu.

Wakati nikiwa kuzimu tulikiwa na televisheni /screen kubwaa, tulkuwa tunaona kila kitu kinachotokea duniani, tulkuwa tunahesabu vitu ambavyo tumeshavifanya kwa sababu tulkuwa tinajua Yesu anaweza akarudi saa yoyote hivyo vyote vitupasavyo kufanya tuwe tumeshafanya, kama madaktari kutokupata dawa ya HIV, na ni kwa sababu wako mwilimi, na nashuhudia leo HIV ilitengenezwa kuzimu ili vijana wafariki wakiwa wadogo kabla hawajajua wokovu wa Bwana Yesu Kristo. Shetani anataka kupata watu wengi atakao ungua nao, bado anaendelea na mashindano na roho ambazo zilimfukuza kutoka mbinguni. Hivyo tulitengeneza HIV na sasa tinaisambaza duniani kote, Lakini hali hizi haziwezi kutibika, iwe ni cancer au TB, madaktari hawawezi kupata tiba, kwa sababu Yesu Kristo yeye pekee ndiye anayeweza kutibu na kuondoa ugonjwa ambao umetemgenezwa kuzimu, mtu ambaye yuko mwilin hawezi kupata tiba kamili, ni Yesu pekee wa Nazareti ndiye anayeweza kutoa tiba kamil, mtu anaweza akaombewa kama anaamini anapona, ugonjwa unainama/bow kwa sababu ya Jina la Yesu, kila kitu kitainama/bow, hata sisi tilkuwa tunainama likitajwa jina la Yesu Kristo


SEHEMU YA II
Hii ni sehemu ya pili ya ushuhuda wa dada NONKOLOSO alyekuwa mfuasi wa shetani.

Nilipo hitimu nltumwa pia kusababisha ajali za ndege, ndege za Australia, Ulaya na sehemu nyingine. Kunapokuwa na ajali ya ndege sio ni kwa sababu ya makosa ya Rubani, ndege zote zilizoanguka najua zilkuwa zinasababishwa na sisi, tulkuwa tunatumwa na hakuna namna tuliweza kukataa, kwa sababu tulkuwa watumwa, tunafanya kazi hata pale ambapo hatukutaka kufanya, tunaambiwa kuwa tutapumzika Yesu akirudi, hivyo kwa kipindi chote lazima tuuwe watu ili Ma-chifu na Shetani, pamoja na wale ambao ndo ma-agent wapya ambao bado hawajaanza kufanya kazi waweze kupata damu, pia tulkuwa tunafanya kazi na wakuu wa nchi na maraisi, sitotaja jina la raisi tulyemkuta, sio mfuasi wa shetani ila tulifanya kazi kwa ajil yake kila siku, alifaulu sheria zetu akarihusu ukahaba, utoaji mimba na kusema kuwa watoto hawatakiwi kuadhibiwa, ilikuwa ni mpango wetu akubali bila kujua kwa sababu tunaona kabisa Yesu yu karibu kurudi,

Tulkuwa tunatuma cham/incantations kila siku kuhakikisha taifa linalaaniwa. Tumefanya kazi sana Africa ya Kusin kama tunavyoona maswala ya utoaji mimba na machukizo mengine, ili watu wajali zaidi kuhusu demokrasia na uhuru wa kujieleza, bila kujua kuwa Yesu yuko mlangoni karibu kurudi, Yesu anatakiwa apate roho nyingi kwa ajili ya ufalme wa Mungu kwa sababu muda karibia unaisha, watoto waliotolewa mimba na mimba zilizoharibika wanalelewa na sisi kizimu, tunawalea afu tunawatumia kwenda kuharibu ndoa, wanandoa watagombana kwa kitu kisichokuwa na msingi, talaka na kutengana na vitu kama hivyo, mtoto alyetolewa mimba ndo kazi zake hizo, kuna wakati muhusika anaweza akaona nyoka nje au ndani inakuwa ni yule mtoto alyetolewa mimba, pia atasababisha ugomvi kati ya ndugu na inaweza kufikia kusababisha vifo.

Ajali ya mwisho ya ndege ya Ulaya nlyosababisha, kulikuwa na mtoto wa Mungu, ambaye alkuwa anaishi maisha ya utakatifu, hivyo damu ilyotokana na ajali ile ilkuwa imeharibika kwa sababu damu ya Mkristo inaharibu damu yote tunayokuwa tunaihitaji, na kama tukinywa inatufanya tukose nguvu ya kuendelea kufanya kazi zetu, hiyo ilkuwa ni ajali ya mwisho ya ndege nilyosababisha, nilisababisha ajali nyingi kama hizo hapo mwanzo na kufanya kazi nyingi kwa ajili ya shetani, baada ya hapo nikawa nimkusanyaji wa taarifa na kufanya zile kazi ngumu kutokana na daraja nililokuwepo, na pia ilkuwa ni jukumu langu kuwaangusha Wachungaji wenye msimamo mkali.

Ngoja nirudi nyuma kidogo kwenye bidhaa zetu, Lacoste (bidhaa zenye picha ya mamba, mara nyingi ni raba za kiume, T-shirt n.k) pia ukivaa kitu chenye nyota, shetani atapanda juu kwenda kuishtaki kwa Mungu kuwa huyu mtu anatembea duniani akiniwakilisha mimi, na huyo mtu ananipenda mimi zaidi ya anavyompenda Mungu, nyota na mamba na viti vyote vyenye miguu miwili iwe ni Tishet, au suruali vyenye picha hizo inaonyesha kutokumuheshimu Yesu ambaye hivi karibuni atarudi, hivyo kama unavyo hivyo ujue unasema kuwa Yesu hana nguvu, sihitaji hata kusema dragon anamwakilisha shetani kwa sababu wengi wanajua, kama unavaa kitu chochote chenye dragon inamwakilisha shetani, na shetani anapanda kwa Mungu na kusema ananguvu kuliko Mungu kwa sababu watu wanatembea duniani wakimwakilisha.

Kwenye swala la code/namba, barcodes zinawakilisha mfuasi wa shetani (satanist), kama mnavyoona kila kitu unachonunua kina barcode (hii ni namba inayowekwa mwenye bidhaa za supermarket), tunatamka laana kwenye vyakula, ndo mana wakristo wanakumbushwa wawe wanafunga, barcodes zote lazima ziwe na namba 3, 6 au 9, ambazo zinawakilisha ulmwengu wa roho, lazima iwe na namba moja wapo kama sio 3 bas 6 au 9, hizi ni namba za kishetani, kabla vyakula havijawekwa kwenye shelfu kuuzwa tunatamka laana/kutambikia vyakula vyote, ombea vitakase kwa damu ya Yesu kabla ya kula.

Kama wewe ni Mkristo na unatumia dawa za mitishamba na za maji kutoka kwa waganga wa jadi bas wewe sio mtakatifu, tutaenda kukushtaki kwa Mungu, kwamba unaabudu vitu tofauti na yeye, Mungu amesema tutawale miti yetu na mimea yote lakin hajasema tuviabudu, havitakiwi kuwa tumaini letu, Yesu peke yake ndiye anatakiwa kuwa tumaini letu, kama utaweka imani yako kwenye dawa za mganga na sio kwa Yesu unatenda dhambi, hizo dawa za mganga zina roho chafu ambazo tumeziweka sisi tutaandika jina lako haraka kwenye kitabu chetu kwa sababu umekuwa wa kwetu.

Wapendwa, kama hujazaliwa mara ya pili na kuokoka, utachomwa motoni, hiyo haikwepeki, wakati nikiwa ndo nmeanza tu kufanya kazi hii ya kumtumikia shetani nlkuwa sijui kama mwisho wa siku ntachomwa motoni, lakini baadae nikagundua. Hizi ni siku za mwisho na zimeongezwa kwa sababu ya neema za Mungu, tulkuwa tunafanya kazi kwa bidii, na kitu kimoja kilchokuwa kimebaki ni kusajiliwa kwa 666, na hiyo itatokea kwa sababu kuna waabudu shetani wengi sana waliokamatwa makanisani na walkuwa wanatoa siri za kule, tukabadili mikakati, badala ya kuwa namba kama wengi wanavyozingatia, bali itakuwa ni namba ya siri ambayo serikali itaipitisha, kama unahizo namba kwenye mkono au kwenye paji la uso basi hutoenda mbinguni, utakuwa kama mfuasi wa shetani, na damu yako itakuwa imejaa namba za kishetani (satanic code)., huo ndo usajili uliokuwa ukingojewa wakati nimeondoka mimi, utafanyika mda wowote kama ilvyo kanisa litakavyonyakuliwa mda wowote, hata tunavyoongea hapa., lakini wote hatujui ni lini mana Mungu ameficha hiyo siku kwa kila mtu,

Tunapofanikiwa kumpata mchungaji wa uwamsho (revival pastor) tunambadilisha kuwa mtumishi wetu bila yeye kujua, atakuwa muabudu shetani bila kutenganishwa na mwili wake, tunaweka roho zetu ndani yao, wakati watu wanakuja kutoa sadaka, tunatamka laana juu ya hizo sadaka kwa njia ya kiroho, hizo laana hazitakuwa juu ya muumini lakini juu ya kanisa, kuna sadaka ya zaka, hii ni ya muhimu sana kwa mwamini, ni asilimia kumi ya mapato, tulkuwa tunawazuiya watu wasitoe zaka, tunawakumbusha kuwa kuna vitu vingi vya kununua na kulipia, baada ya hapo tunaenda kukuishtaki kwa Mungu kuwa unamuibia hela yake,

Tunamwambia Mungu kuwa mahitaji ya huyu muumini ni ya muhimu kwake kuliko Mungu, Shetani atakuita mwizi kwa sababu umeiba hela ya Mungu na hujailipa yote, nakushauri chochote unachotakiwa kutoa kwa ajili ya Mungu toa, ni asilimia kumi tu ya mapato yako. Kutoa zaka itakulinda na ajali na kukusaidia kuwa mtakatifu. Ni muhimu sana ulipe zaka kabla ya kuanza kufanya mambo yako mengine, huwezi kuruka mwezi mmoja afu useme mwezi unaofuata utalipa mara mbili, mwezi uliorukwa tayari ni laana, haiwezi kubadilika kuwa baraka baada ya kufidia mwezi unaofuata, kama unakumbuka vzr Mungu alimtoa mwanae wa pekee, haikuwa rahisi au kitu kizuri, lakini alifanya hivyo ili usiende kuzimu, na wewe lazima utoe kwa ajili ya kazi yake.

Wakati mtu anakaribia kufa, tutamtembelea, kuna watu huwa wanafikiri watatubu dhambi zao wakiwa wagonjwa na wakiwa karibia kufa, huwa tunaenda na kuwafunga midomo yao ili wasiweze kuungama dhambi zao, huwezi kutubu dhambi zako moyoni tinahitaji midomo kufanya hivyo kama anavyofanya mtu akizaliwa mara ya pili/kuokoka, anatakiwa kukiri kuwa Yesu Kristo ni bwana kwa kinywa chake, hivyo mtu huyo akifa na dhambi zake tutaandika jina lake kwenye kitabu chetu na atachomwa pamoja na sisi. Watu wanaokufa katika dhambi, watu hawa ndo tunaowatumia kurudi kuwasumbua ndugu zao, tunatumia mifupa yao na kujigeuza na kutokea kwa ndugu zao kama wao na kuwaambia mambo ya kufanya, nao watafanya wakijua ni kumuheshimu ndugu yao alyefariki,

Lakini inakuwa ni sisi, tunaweza tukaweka hela mahali maeneo ya nyumbani na kumwambia huyo mtu kuna hela pia iko sehemu fulani, na wataamini kuwa huyo ndugu yao alyefariki anawasaidia, hivyo ndo tulvyokuwa tunafanya ili watu waamini ibada za mizimu. Hata kama ni mwamini pia tunaweza kukutokea, mana kuna waamini ambao wanaanguka katika nyakati zao za mwisho kuishi duniani, katika dakika ya mwisho watataka mnyama achinjwe kwa ajili ya heshima kwa mizimu, hapo hapo tutaandika jina la mtu huyu kwenye kitabu chetu, kuwa amekufa akiwa anafanya ibada ya mizimu, tunaangalia watu kabla ya kufariki na wengine wanaanguka, kama umekufa kwenye utakatifu hatuwezi kutumia mifupa yako kwa ajili ya kudanganya ndugu zako, kwa sababu itakuja kufufuliwa wakati Yesu atakaporudi.

Baada ya muda kupita, kuna mchungaji mmoja mwenye upako anaitwa Chiliza kutoka Mandawe, nilianzaga kumfuata kabla hata sijahitimu, wahati nilipohitimu niliambiwa nishughulike nae kwa sababu alkuwa na msimamo mkali sana na upako, anaombea watu wenye HIV wanapokea uponyaji na wanaotembelea baiskeli wanaweza kunyanyuka kutembea, tulianza kuwaambia watu kuwa ni mfuasi wa shetani na anatumia uchawi kufanya hiyo miujiza na watu walkuwa wanatuamini. Niliahidiwa zawadi ya gari aina ya NISSAN NAVARRA, kama nikifanikiwa kumwangusha mtu huyo wa Mungu, na anapoanguka hatumzuii kuendelea kuhubir anaendelea lakin atatumika na roho wachafu ili afundishe mafundisho yanayowachanganya watu n.k., hivyo watu wote waliookoka (wapya) watakuwa kwenye mitego kutokana na mafuandisho yake, kwa sababu ataanza kufundisha nusu ya ukwel na atakachojisikia yeye kufundisha, ninapofika kwenye kanisa lolote huwa nakaa nyuma, kuangalia kwanza nini kinaendelea, nasoma maisha ya mchungaji, kwa sababu kama nataka kimuangusha kwanza lazima nimsome ni mtu wa namna gani, ntatafuta udhaifu wake uliko akiwa kazin au nyumbani,

Mchungaji Chiliza wakati ameanza semina ya uamsho maenea ya ufukweni mwa bahari nilkuwa bado namfuatilia, akiwa anatoka kwenda kuwahubiri watu habari njema waokolewe nilkuwa bado niko sambamba nae, mwaka 2008 alkuwa na mkutano wa uamsho pale FUSCADALE, hapo ndipo nilpoweza kumsoma vizuri, na kulkuwa kuna ukuta wa moto umemzunguka, kama wewe ni mtoto wa Mungu na umeokoka kwel na unafunga mara kwa mara unakuwa unalindwa na ukuta wa moto kukuzunguka, nilipita nyuma yake nikaenda nyumbani,

Mchungaji Chiliza alkuwa na semina ya uamsho KHUSHWINI, na nililazimishwa kuvaa mwili wangu wa bandia, kwa sababu ilkuwa ni karibu na nyumbani kwangu, namba yangu ilkuwa kwenye damu yangu, nilienda pale na rafiki yangu Slindile, yeye sio muabudu shetani, na alkuwa hajui kama mimi ni wakala wa shetani, alkuwa amefungwa na roho za kichawi na tulkuwa marafiki wazuri, nilkuwa natengeneza watu nywele, na tulkuwa na nywele ndefu za bandia, nlkuwa nasuka mwenyewe na tulkuwa tumesuka mtindo wa aina moja, sikiliza maonyo yangu ninaposema nywele bandia ni hatari, tulfika na gar pamoja na waumini wengine ambao walkuwa hawajui kama mimi ni wakala wa shetani hata rafiki yangu hakuwa anajua, alkuwa mkali na sio mtiifu nyumbani kwao ndo mana alkuwa rafiki yangu, na nlkuwa namshauri vibaya, tulikaa nyuma na mtumishi wa Mungu alfika na mke wake, alipoingia tu, alsema kuna roho mchafu mahali pale, alkuwa ni nabii pia, rafiki yangu akaruka na kuanguka chini alkuwa anataka akimbie, Nilkuwa nampenda sana rafiki yangu, na tulikuwa wakorofi, watu tuliokuja nao kwenye gari ni mashaidi wanajua ni jinsi gani tulkuwa wajeuri, nilmchukuwa rafiki yangu nikampeleka mbele madhabauni akaombewe kwa sababu nlkuwa sitaki mtu yoyote amshike maana tulkuwa na majivuno sana, nlkuwa najiaminisha kuwa mimi ni muhitimu na siwezi kuzidiwa nguvu kutokana na daraja nlilokuwa nalo, na nlkuwa namlinda Chifu (alyekuwa wakala wa shetan akafariki duniani jina lingine anaitwa Satanist) asiungue na maombi yenye moto, na namba yangu/code ilkuwa ndani yangu, Mchungaji Chiliza akauliza nani yuko na huyu binti alyedondoka?

Hapa ni kabla hajaanza kuhubiri, nikamjibu kwamba ni mimi ndo niko nae, aliendelea kuhubiri, na akarudia swali lake sikuweza kufungua mdomo, Roho mtakatifu alyekuwa ndani yake alisababisha nguvu zangu ziishe, sikuweza hata kunyanyua mguu wangu, aliuliza tena na sikuweza kujibu, akawageukia waumini na kuwaambia angalieni hichi kitu, akatamka kwa nguvu MOTO, ni kweli Yesu ni moto unaochoma, alposema hivyo kwenye ulimwengu wa roho niliona moto unamiminika kutoka machoni mwake, mikononi, mdomoni, nikadondoka chini na shetani akanichukuwa kutoka kwenye mwili wangu haraka na kunipeleka kuzimu halafu shetani ambaye anaumiliki mwili wangu akabaki pale. Wakati pepo anahangaika kwa sababu ya moto anajibu swali lolote, wachungaji wengi hawajui hiki kitu, kama usipounguza code/namba kutoka kwenye mwili wa mtu, anabaki kuwa wakala wa shetan hata baada ya kuokoka, kwa haraka Mchungaji Chiliza akagundua hili, akamwamuru pepo ataje ile namba na akaichoma kwa moto wa Mungu, pale tu ile namba ilipounguzwa, shetani kule kuzimu alkuwa hana namna zaidi ya kumiachia, pepo ambaye alkuwa ndani yangu akarudi kuzimu, kama wasingeunguza ile code kwenye mkono wangu, shetani angeweza kuniita tena kwa sababu sikuwa naitwa kwa jina langu bali ni kwa ile namba, namba ya mwisho ambayo niliipokea baada ya kuhitimu ilitoka na damu, baada ya kuombewa nilirudi kwenye hali yangu ya kawaida na nikafanya maamuzi ya kuokoka na kushuhudia ulimwenguni kote, namwamini Mungu kwa sababu nimeona nguvu zake, najua ananguvu zaidi ya shetani

Kabla sijasahau baada ya unyakuo dunia haitaisha, kutakuwa na kanisa moja ambalo watu wote watalazimishwa kwenda kusali humo, sitosema jina la hilo kanisa ila tayari kanisa hilo lipo, watu ambao hawajanyakuliwa watalazimishwa kwenda huko kumwabudu mpinga Kristo, hili kanisa lipo.. Tubu na ujiandae Yesu yu karibu kurudi.

Ushuhuda huu umetolewa kwenye anwani hiyo hapo chini, ukatafsiriwa kwa Lugha ya kiswahili ili habari hizi ziweze kuwafikia watu wengi zaidi.

Follow up Holy End times teachings and also other testimonies; www.holybridesaints.wordpress.com
Facebook page = holy bride saints
Email; gichingas@gmail.com
Youtube channel= Watchman Peter
+254703274922 @ Whats app/Telegram.USHUHUDA WA ALIYEKUWA WAKALA WA SHETANI.


Mawasiliano yetu kwa huduma mbalimbali za maombezi personal life Tafadhali usisite Kututafuta kupitia HiZi social media
WhatsApp and phone number is +255756717689 pia Unaweza kukupigia kupitia no hii
Facebook Mt D. Makubi
Instagram Mt Daudi Makubi
Twitter Mt Daudi Makubi
Website mtdaudimakubi.blogspot.com
Email address makubimsafiri@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA YA NAFSI, ROHO, MOYO NA MWILI.?

BWANA YU PAMOJA NAWE EE SHUJAA