INAWEZEKANA KABISA MWANAUME KUWA NA MWANAMKE MMOJA
INAWEZEKANA KABISA MWANAUME KUWA NA MWANAMKE MMOJA
Yaani sisi ni tai, ila hatuelewi, tunajifahamu kama kuku. Kwamba tunao uwezo mkubwa wa kuwa mwanaume wa mwanamke mmoja lakini tumeaminishwa kinyume chake tumeamini na tunaishi ndani ya uongo huo uliopikwa vizuri.
Mkulima mmoja aliokota yai la ndege tai akalichukua na kwenda kulichanganya na mayai ya kuku wake aliyekuwa anatamia. Baada ya muda kuku akatotoa pamoja na lile yai la tai.
Mama ambae ni kuku akamlea tai akijua ni mtoto wake, Tai akakua pamoja na vifaranga vya kuku, Akachakura jalala moja akitafuta chakula kama vifaranga wengine, Akienda huku, ‘kampani’ yake ilikuwa ni kuku, akirudi huku ‘kampani’ yake ilikuwa ni kuku.
Siku moja, akiwa na kuku wengine akaona familia ya tai inapaa angani. Akatamani kuwa mmoja wa wale tai, kuwa kule juu, mawinguni akamgeukia kuku mmoja aliyekuwa karibu yake, akamwambia. “Natamani ningekuwa tai.”
“Haitawezekana.” Kuku akamjibu, kisha akaongeza. “Wewe umeumbwa kuku, na utabaki kuwa kuku milele daima. Kutamani kuwa tai ni kama kupiga mluzi huku unatafuna karanga, Haiwezekani.”
Basi tai aliendelea kuishi kama kuku hadi kufa kwake, lakini yote ilikuwa ni kwa sababu ndogo tu aliamini uongo aliokuta tangu alipozaliwa.
Uongo kama wa hadithi ya tai na kuku tunaishi nao wanaume. Tumezaliwa tumekuta hadithi inayosema kwamba, hakuna mwanaume wa mwanamke mmoja Na tumeamini.
Yaani sisi ni tai, ila hatuelewi, tunajifahamu kama kuku. Kwamba tunao uwezo mkubwa wa kuwa mwanaume wa mwanamke mmoja lakini tumeaminishwa kinyume chake tumeamini na tunaishi ndani ya uongo huo uliopikwa vizuri.
Uongo uliotengenezwa kwa shahidi za kila namna. Za kijamii, kidini, kihistoria na kibailojia.
Kijamii utaambiwa kwamba wanawake wako wengi kuzidi wanaume, kwa hiyo ili kuhakikisha kila mwanamke anahudumiwa, inatulazimu wanaume tuwe na mwanamke zaidi ya mmoja. Tumeamini. Na hapo bado kuna uongo uliofichwa kwenye mila na desturi tele za hovyo.
Kidini utaelezewa kuhusu watu ambao sisi ni wafuasi wao, jinsi walivyokuwa na wanawake zaidi ya mmoja tena wengine wakipewa kibali cha kufanya hivyo na Mungu. Inatia ukakasi, lakini imewekwa vizuri kuaminika kwa urahisi ikiwa unayechukulia mambo juu juu.
Wakati kihistoria utaambiwa jinsi mashujaa wa zama hizo walivyokuwa mashujaa pia kwenye suala la kumiliki warembo wengi wengi. Utapewa majina ya Machifu wazito, na utaambiwa idadi ya kushangaza ya wanawake waliokuwa wanawamiliki kana kwamba ilikuwa ni bidhaa na watakushangaa kwamba inawezekanaje rijali unakuwa na mwanamke mmoja.
Kama mwanaume, kuwa na wanawake zaidi ya mmoja ni utumwa. Utaishi maisha ya kufuta meseji kila jioni kabla ya kuingia kwa mkeo na Maisha ya kuhudumia familia mbilimbili ambazo ni mzigo na wote tunajua hili.
Lakini maisha ni maamuzi unaweza kuendelea kuwa tai aliyekuta uongo wa kwamba yeye ni kuku, Au kuwa tai ambaye anafahamu yeye ni tai, na akawa huru kwa kuruka mbali kabisa na uongo uliopikwa ili kumuangamiza kwa taswira ya kumpa sifa.
Ninatamaini umejifunza kitu cha muhimu sana ktk maisha ni mimi Mt Daudi Makubi kwa mafundisho zaidi karibu hapa na Wasiliana nasi kwa mawasiliano hapo chini.
Ukurasa wetu wa facebook ni mwinjilist e Daudi Makubi
Twitter Mt Daudi Makubi
Instagram Mt Daudi Makubi
Facebook Mt Daudi Makubi
WhatsApp no +255756717689
Email makubimsafiri@gmail.com
Nimekuelewa mtumishi naomba nisaidie kitu hapa nawengine wajue niwapi biblia imekataa kuwa na wanawake zaidi ya mmoja
ReplyDeleteMafarisayo walimwendea Yesu wakamwambia ni haki kumuandikia talaka mwanamke?
DeleteYesu tokea mwanzo Mungu alimuumba mwanaume mmoja na mwanamke mmoja lkn kutokana na ugumu mioyo yenu musa akawaruhusu kupeana talaka.
Maongezi haya kati mafarisayo na Yesu yanatufundisha nini sisi wakristo wa leon?
Inamaana kwamba mpango wa kwa mwanadam juu ya mahusiano ni ya mwanamke mmoja kwa mwanaume mmoja lkn tamaa za mwanadam ndizo zinazozalisha uwingi kutaka kuna mwamke zaidi ya mmoja.
Mafarisayo walimwendea Yesu wakamwambia ni haki kumuandikia talaka mwanamke?
ReplyDeleteYesu tokea mwanzo Mungu alimuumba mwanaume mmoja na mwanamke mmoja lkn kutokana na ugumu mioyo yenu musa akawaruhusu kupeana talaka.
Maongezi haya kati mafarisayo na Yesu yanatufundisha nini sisi wakristo wa leon?
Inamaana kwamba mpango wa kwa mwanadam juu ya mahusiano ni ya mwanamke mmoja kwa mwanaume mmoja lkn tamaa za mwanadam ndizo zinazozalisha uwingi kutaka kuna mwamke zaidi ya mmoja.