KILA KONA IMEKUWA ((COVID-19

DUH KILA KONA IMEKUWA ((Covid-19 Corona virus)) tambua Kabla ya corona kifo kilikuwepo na baada ya corona pia kifo kitakuwepo, Jitathimini ulipotoka, ulipo na unakokwenda. 

2Wathesalonike 3:3 Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu. Utafanywa imara utalindwa na mwovu kwa shalti moja tu la kumpa YESU maisha yako nje ya YESU hakuna usalama aise!!! 


Ndugu yangu mpendwa hivi ni kweli hivi ndivyo ulivyo?

Ziko wapi nguo zako na viatu vyako vizuli?
Iko Wapi gari yako V.X V.8🚗 uliyotamba nayo ukawamwagia watu maji Barabarani?
Kwanini haupo kwenye nyumba yako nzuli ya thamani?
Ngoja kwanza!! ziko wapi zile sherehe ulizokuwa ukizifanya na kusherekea kila kuchwapo?

Iko wapi Digrii yako na Masters?
Iko wapi passport yako na Visa?
Mbona hauna hata ile ATM card 🏧 yako?
Ooooh nini kimetokea kwenye meno yako na dimpozi zako?
Iko wapi ile iPhone uliyoipenda Sana?
Ziko wapi kumbukumbu zako za bank 🏦 (Bank statement)?
Hivi nini kimetokea kwenye staili yako ya nywele?
Ziko Wapi zile nywele za kibrazili vilizo vutia na kukufanya mrembo?

Jamani liko wapi lile umbo no 8 na urembo wako wote?
Aise utanashati wako wote uko wapi?
Kuko wapi kujipodoa kwako na ule urembo wa kucha duh?

Hakika maisha ya duniani yote ni upepo tu mpendwa wangu.
Ishi maisha yenye hofu ya MUNGU, na ndipo utakapo ona duniani ni sehemu nzuli, acha kuwa na Kiburi, Ubinafsi, Chuki, Majivuno, na Dharau.!

Ishi maisha ya kumpendeza MUNGU Biblia inasema katika
1Wakorintho 13:4
Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

Nyenyekea onyesha Ubinadam kwa kila mtu kwa kutenda mema unaweza ukakaribisha Malaika pasipo kujua, lkn pia ni moja ya njia ya kumuhubiri Kristo kwa matendo yako mema na wengi wameokoka kwa njia ya kama Hiyo Paulo Anasemaje
1Wakorintho 13:3
Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
Kumbe unahitajika upendo utokao ndani ya moyo yaani usichopenda kutendewa basi nawewe usimtendee mtu, Upendo Ndio tunda la Roho.
OOOOOH LIFE...........LIFE........ALL IS VANITY.

Kweli kufa kupo lkn unakufaje?
Umeandaa maisha yako ya kesho, unajua Uendako, Uhakika upo ktk DAMU YA YESU PEKEE, Mwana (yaani YESU) hakuja ili auhukumu ulimwengu bali ulimwengu uokolewe kupitia yeye, bado unayo nafasi ya kutubu na kutengeneza njia zako mpe YESU maisha yako ili siku moja uuridhi uzima wa milele pamoja na watakafu, Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu.Waebrania 10:19

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA YA NAFSI, ROHO, MOYO NA MWILI.?

USHUHUDA WA ALIEKUWA WAKALA WA SHETANI

BWANA YU PAMOJA NAWE EE SHUJAA