KAMA GIDIONI
1. Kama Gideon,
baadhi yetu tumefichwa na matatizo ambayo sisi ndio tunapaswa kuyatatua.
Tunazikimbia changamoto ambazo tuliumbwa ili tuzitatue.Toka Huko Mafichoni Aisee!
2. Wewe usipodhihirika, wengi wataathirika.
Wito wa Mungu kwako ni muhimu sana, Hupaswi kuupuuzia.
Viumbe vyote vinakusubiria udhihirike, tambua hilo, na Chukua hatua.
3. Weka woga kando, weka hofu kando, katika nchi yako ya ahadi lazima kuna majitu, lakini hayataweza kukudhuru.
Wewe na Mungu ni jeshi kubwa, nenda kwa imani,
nawe utaangusha milki za wafalme, na kuimiliki nchi yako ya ahadi.
4. Usikubali kukata tamaa. Usikubali kurudi nyuma.
Usikubali kuvunjika moyo. Labda kwa wanadamu haiwezekani,
lakini si kwa Mungu; ukiwa na Mungu, yote yanawezekana.
5. Wakati mwingine tunapitia mambo yanayotuumiza katika maisha,
lakini mambo hayo hayo ndiyo yanaweza kuwa yanatuonesha kusudi na wito wa Mungu kwetu.
Jiulize, mapito haya yatanifaa wapi?
KUSUDI LAZIMA LITIMIE!
Makubimsafiri@gmail.com
https://mtdaudimakubi.blogspot.com/2019/12/kama-gidioni.html
ReplyDeleteUsikubali kukata tamaa. Usikubali kurudi nyuma.
Usikubali kuvunjika moyo.
Labda kwa wanadamu haiwezekani,
lakini si kwa Mungu; ukiwa na Mungu,
Yote yanawezekana.