Posts

USHUHUDA WA ALIEKUWA WAKALA WA SHETANI

Image
USHUHUDA WA ALIYEKUWA WAKALA WA SHETANI. (Umetafsiriwa) Wapendwa rafiki zangu, napenda kuwashirikisha ushuhuda huu wa binti kutoka South Africa alyekuwa wakala wa shetani, alkuwa mtumishi wa shetani kwa miaka kumi na miwili na alpandishwa cheo akiwa huko. Nawasalimu kwa jina la Yesu Kristo, jina langu ni NONKOLISO NGELEKA kutoka Nzimakwe, nmefanya kazi mahali pale kwa miaka 12, nimezalia mwaka 1988, Nilifanya kazi mahali pale tangia nikiwa bint mdogo kadiri muda unavyoenda nikazidi kupanda daraja, kuna madaraja tofauti, kuna waabudu shetani makanisani bila kujua kama wanamwakilisha shetani, na wapo waabudu shetani ambao wanaweza kujitenganisha na miili yao yakawaida na kuwa kwenye ulimwengu wa roho (kama wachawi wanavyofanya), mimi nilkuwa kwenye kundi la pili la wanaojitenganisha n miili yao. Nilianza kuwa napata ndoto nikilala naota napigana kama ilivyo kwenye michezo ya kuigiza kwenye televisheni wakiigiza wanapigana maeneo ya mjini halafu kama wanapaa juu, baada ya sik...

HADITHI YA MDADA KIPOFU

Image
HADITHI YA MDADA KIPOFU Hapo zamani kulikuwa na Mwanamke kipofu ,alie chukia sana hali yake ya kuwa kipofu, alimchukia kila mtu kwakweli ikiwemo nduguze na wazazi wake isipokuwa Mchumba wake, alie mpenda na kumjali nakuwa nae wakati washida na raha hivyo alimthamini, alilia kilasiku na kujisemea kuwa SIKU ikitokea akaona Basi jambo la kwanza lingekuwa ni KUFUNGA NDOA na Mchumba wake huyo aliempenda sana na kumfanya kila kitu ktk maisha yake.... (kumbuka hii ni hadithi) Siku Moja alipata Bahati ya KUKOPESHWA Macho, ambapo aliweza kuona kila kitu kilicho kuwa mbele yake, Pamoja na Boyfriend Wake nae Boyfriend wake aliitunza ahadi ya mchumba wake sasa baada yakuwa sasa anaona alimuomba kama itawezekana sasa WAOANE Kama Alivyo AHIDI. Mdada huyo alishitushwa na hali aliyokua nayo Mchumba wake huyo maana Nayeye kumbe alikua KIPOFU pia kama alivyo kuwa yeye hapo kabla, mdada huyo alikataa KUOLEWA na Kijana kipofu aliejitoa na kuthamini kama nafsi yake, Boyfriend wake aliondoka huku M...

TOFAUTI KATI YA WATU WALIOFANIKIWA NA WASIOFANIKIWA

Image
Mafanikio ni aina ya tabia fulani ambayo mtu huijenga na haiji tu kwa bahati mbaya bali ni mpango mkakati unaopaswa kuwa nao maishani tofauti na hivyo you can kiss goodbye mafanikio leo tutaangalia hasa vitu vikuu vitatu vilivyobeba watu wanaofanikiwa na wasio fanikiwa. Wote tunakuja duniani baada ya kuwa washindi katika mapambano makubwa yanayohusisha mamilioni kwa mabilioni ya washiriki Wote tunakaa mapumzikoni miezi tisa tukijaandaa na pambano lingine, Wote tunakuja duniani tukiwa full packed na vitu muhimu vya kutusaidia kushinda mapambano mengine ya hapa duniani, ambapo Mungu humpa kila mtu vitu sahihi anavovihitaji kuendana na aina ya pambano lake, Yaani tunapewa vitu kama vile Passion, talents, core abilities, potential, akili, nguvu, viungo kutokana na kuendana na aina ya mapambano unayoyaendea, SWALI NI JE, NINI KINASABABISHA WENGINE WASHINDE MAPAMBANO YA HAPA DUNIANI NA WENGINE WASHINDWE ILI HALI WE ARE ALL WINNERS?? (Sisi wote ni washindi) Utofauti huanza kuonekan...

BWANA YU PAMOJA NAWE EE SHUJAA

Image
BWANA YU PAMOJA NAWE EE SHUJAA Waamuzi 6:12-16 12-Malaika wa BWANA akamtokea, akamwambia, BWANA yu pamoja nawe, Ee shujaa. 13-Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye BWANA, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani. 14-BWANA akamtazama, akasema, Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma? 15-Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu. 16-BWANA akamwambia, Hakika nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kama mtu mmoja. Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu, ninatamani sana uyajue mapenzi ya Mungu na Kusudi kuu la wewe kuwapo hapa duniani maana haupo duniani kwa bahati mbaya. Huwa namfurahia Mungu sana na nguvu zake n...

ILI UFIKIE KILELE CHA NDOTO ZAKO NI LAZIMA MANENO HAYA MANNE YASITOKE KINYWANI MWAKO.

Image
ILI UFIKIE KILELE CHA NDOTO ZAKO NI LAZIMA MANENO HAYA MANNE YASITOKE KINYWANI MWAKO. Bado tunamuangalia Dr. Myles Munroe kama model wetu siku ukitaka kupata hatua ya jambo lolote jifunze kwa walio fanikiwa sio ushamba wala ujinga ila ndivyo maisha yalivyo kupitia wao tunapata aidia Mpya au mawazo mapya. 1. Usiangalie udhaifu wako bali angalia pale una NGUVU. Kila mtu aliyezaliwa na mwanamke ana madhaifu, Tofauti ni huwa kwenye namna ya kudeal na madhaifu aliyo nayo. Tabia kuu ya watu wanaofanikiwa ni kwanza kuyakubali madhaifu yao na baada ya hapo ni kutojisumbua kupoteza muda na nguvu kwenye madhaifu yao kwani wanajua kuwa ili uitwe binadamu ni lazima uwe na madhaifu kwenye maeneo fulani fulani na sio dhambi kuwa na madhaifu hayo maana huko ndio kuukamilisha ubinadamu, Na wanatambua kuwa kupambana na madhaifu yao ni kupoteza nguvu za kupambana kuhusu Ndoto zao, Kubali Madhaifu yako na Wekeza nguvu nyingi kwenye STRENGTH zako. Kitu cha msingi unachotakiwa kufanya ni kuhak...

ISHI KWA KUTUMIA UWEZO AU NAFASI YAKO YOTE ILI UFE UKIWA UMEKAMILISHA KUSUDI HUSIKA HAPA DUNIANI.

Image
ISHI KWA KUTUMIA UWEZO AU NAFASI YAKO YOTE ILI UFE UKIWA UMEKAMILISHA KUSUDI HUSIKA HAPA DUNIANI. Wakakati mwingine huwa naamka nimechoka naona kama siwezi kusonga mbele zaidi, Siku zingine najihisi kukata tamaa na kuwaza kuacha ninachokifanya, Sometimes naona ugumu mkubwa sana ndani yangu, lakini wakati mwingine naona kama ninavovifanya kwa ajili ya jamii kama najiumiza tu na hakuna faida ninayoipata, naona kama najipotezea muda vile, Inafika hatua nachoka sana nakata tamaa kabisa, wakati mwingine naona kama maumivu ninayoyapata ni makali sana, Inafika hatua nakosa hamasa ya kuendelea mbele, nakosa nguvu za kusonga mbele, Inafika hatua najihisi mnyonge asiye na nguvu za kuendelea hata kwa moja mbele zaidi, Sometimes naona kama ndoto zangu ni kubwa sana siwezi kuzitimiza na nakosa nguvu kabisa na hamasa ya kuendelea mbele. Lakini kila nikipitia kipindi kama hiki huwa naisikia sauti nyembamba sana na ya upole ikinikumbusha maneno aliyokuwa akiyasema Dr. Myles Munroe maeneo mbali...

Prisca_Sanga_Sikuachi