ISHI KWA KUTUMIA UWEZO AU NAFASI YAKO YOTE ILI UFE UKIWA UMEKAMILISHA KUSUDI HUSIKA HAPA DUNIANI.

ISHI KWA KUTUMIA UWEZO AU NAFASI YAKO YOTE ILI UFE UKIWA UMEKAMILISHA KUSUDI HUSIKA HAPA DUNIANI.

Wakakati mwingine huwa naamka nimechoka naona kama siwezi kusonga mbele zaidi, Siku zingine najihisi kukata tamaa na kuwaza kuacha ninachokifanya, Sometimes naona ugumu mkubwa sana ndani yangu, lakini wakati mwingine naona kama ninavovifanya kwa ajili ya jamii kama najiumiza tu na hakuna faida ninayoipata, naona kama najipotezea muda vile, Inafika hatua nachoka sana nakata tamaa kabisa, wakati mwingine naona kama maumivu ninayoyapata ni makali sana,

Inafika hatua nakosa hamasa ya kuendelea mbele, nakosa nguvu za kusonga mbele, Inafika hatua najihisi mnyonge asiye na nguvu za kuendelea hata kwa moja mbele zaidi, Sometimes naona kama ndoto zangu ni kubwa sana siwezi kuzitimiza na nakosa nguvu kabisa na hamasa ya kuendelea mbele.

Lakini kila nikipitia kipindi kama hiki huwa naisikia sauti nyembamba sana na ya upole ikinikumbusha maneno aliyokuwa akiyasema Dr. Myles Munroe maeneo mbalimbali, alikuwa akisema "Utajiri mkubwa duniani hauko kwenye visima vya mafata vilivyopo Uarabuni, wala migodi ya dhahabu iliyopo Afrika Kusini, Bali utajiri mkubwa duniani upo MAKABURINI,

Alikuwa anaendelea kwa kusema Makaburini wamelala watu ambao walitakiwa kuimba nyimbo nzuri lakini hawakuimba hata wimbo mmoja, Wamelala watu ambao walitakiwa kuwa viongozi wakubwa wa kitaifa ila wamekufa wakiwa hawajawa hata viongozi wa vitongoji, Wamelala watu ambao walitakiwa kuwa watunzi wa vitabu, nyimbo, mashairi lakini Wamelala na vitu vyao, wamelala watu ambao walitakiwa kugundua vitu vingi vipya katika dunia yetu lakini wamelala hawajagundua chochote,

Wamelala watu ambao walitakiwa kuwabadilisha wengine in a positive way lakini wamelala hawajabadilisha mtu hata mmoja, Wamelala watu ambao walitakiwa kuanzisha biashara mpya na kubwa lakini wamelala hawajaanzisha hata kioski, Kisha anasema "Hazina" "Thamani" na "Utajiri" uliozikwa Makaburini "unamfanya MUNGU ahuzunike kila siku" alikuwa anamaliza kwa kusema
"DIE EMPTY" YAPE HASARA MAKABURI!!

Kila nikiyafikiria maneno haya huwa napata nguvu na sababu ya kuamka tena na kusonga mbele, huwa napata strong reason ya kuendelea kufanya vitu kwa ajili ya jamii, huwa napata nguvu ya kuinuka tena, kusimama na kuendelea kusonga mbele!!
NAPATA UJASIRI MKUBWA WA KUSONGA MBELE NA NISEME TU KUWA KILA NIKIYAKUMBUKA HAYA MANENO NAKUWA KWENYE  UNSTOPPABLE STATE!!

Hali hii inayonitokea huwa inamtokea kila mtu kwenye maisha yake, kama ukipata chance ya kumuuliza mtu yeyote aliyefanikiwa basi atakwambia hali hii imemtokea mara nyingi sana, lakini uwezo wa kuwa na sababu ya kuendelea mbele, Sababu ya kukutia nguvu, Sababu ya kukupa hamasa ndicho kitu pekee kitakachokufanya uendelee kufanya unachokifanya kwa ajili ya ndoto yako.

JE, NI SABABU GANI INAYOKUPA NGUVU YA KUENDELEA KUSONGA MBELE PALE UNAPOKUTANA NA HALI YA KUKATA TAMAA YA KUENDELEA NA MAPAMBANO YA NDOTO YAKO?? Sababu ndo kitu cha pekee kitakachokufanya Uendelee kusonga Mbele!! Bila sababu huwezi kuendelea mbele lazima uwe na (mzigo) sababu inayokupushi

Sasa ili kuungana na watu wachache ambao wameamua kuyafirisi na kuyapa hasara makaburi (DIE EMPTY) na kuungana na watu kama Dr. Myles Munroe, Martin Luther King Jr ni lazima ufanya mambo mawili yafuatayo:

1. Usikubali kuridhika na vitu ulivyofanya hata kama ni vizuri na vikubwa kiasi gani hesabu kama hujafanya chochote,

Kuridhika ni adui mkubwa sana wa maendeleo yako na mafanikio yako, kuridhika kumesababisha watu wengi wafe wakiwa FULL!! (Wajinga) Kuridhika kumezalisha watu wengi wa kawaida ambao ilitakiwa wawe Wakuu sana lakini wakabweteka kwa vichache au vingi ambavyo ilikuwa bado sio FULL POTENTIAL,

Kuna msemo unasema "kuridhika na mafanikio yako ya sasa ndo adui wa mafanikio yako makubwa au ya kesho" Get out of your comfort zone!! Keep pushing, Keep Grinding!! USIKUBALI KURIDHIKA PAMBANA TILL THE LAST DAY!!

USIKUBALI KURIDHIKA KAMA WENGINE WENGI WALIVYORIDHIKA AMUA KUJITOFAUTISHA AMUA KUWA TOFAUTI!!
Usikubali kuwa wa kawaida, amua kuwa wa tofauti, shida watu wengi wanaogopa kufanya vitu vya tofauti kwa kuogopa watu watawasema, Usikubali kuwa wa kawaida, usikubali kuwa kama wengine wengi walivyo amua kuwa kama wengine wachache walio tofauti na wengi,

"Decide to be different" Watu wakikuuliza Kwanini unapenda kujifanya wa tofauti wewe? Waambie "God created me different from others" "MUNGU AMENIUMBA TOFAUTI NA WENGINE" kwa kazi maalum na napenda kuwa wa tofauti ili dunia uwepo wangu uwe na maana, Kumbuka kuwa Thamani yako ipo kutokana na utofauti wako na Mungu anafurahia wewe kuwa tofauti na wengine kwani alikuumba tofauti, hili ni jambo la kwanza na la pili ni hili........!

2. Amua kutumia "Gifts" "Talents" "Abilities" ulizopewa na Mungu kila siku ya maisha yako kumbuka hilo.

Kama unaweza kutunga mashairi tunga kila siku, kama unaweza kuandika vitabu basi andika kadri uwezavyo, kama unaweza kushauri basi shauri kwa nguvu zote, kaka unaweza kuigiza basi igiza mpaka mwisho, kama umezawadiwa kufundisha fundisha kwa nguvu zote bila kuchoka,

Kama unaweza biashara basi fanya biashara kwa nguvu zote, kama unaweza kuimba basi Hakikisha unaimba kwa nguvu zote na mara nyingi iwezekanavyo, KILA KITU AMBACHO UNAFANYA HAKIKISHA UNAFANYA KWA NGUVU ZOTE, KWA KUJITUMA BILA KUCHOKA WAKA KUACHA MPAKA SIKU YA MWISHO!!

Myles Munroe alifariki akiwa anaelekea sehemu kutoa semina na kufundisha, Yaani amekufa akiwa anapambana kufa Empty, Amekufa akiwa ana Push to the Limit!! Yaani ni Vizuri sana mauti ikukute ukiwa unatumikia Kusudi la Kuumbwa kwako!! AMUA KUANZIA LEO KUWA HATA UPITE KWENYE UGUMU NA HALI YA KUKATISHA TAMAA KIASI GANI UTAKUFA UKIWA UMETUMIA UWEZO WOTE MUNGU ALIOUWEKA NDANI YAKO
"DECIDE TODAY YOU WILL DIE EMPTY"

Live in  Your Dream completely
Mt Daudi Makubi

Like page yetu na follow account yangu ili kuendelea kujifunza zaidi.
Facebook page: mwinjilist e Daudi Makubi
Facebook account: Mt Daudi Makubi
Phone number +255756717689
Email makubimsafiri@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

NINI MAANA YA NAFSI, ROHO, MOYO NA MWILI.?

USHUHUDA WA ALIEKUWA WAKALA WA SHETANI

BWANA YU PAMOJA NAWE EE SHUJAA