USIOGOPE
Maisha ya mwanadamu siku zote ni tegemezi na katika kutegemea, inategemea unaamini nini katika maisha yako,
Maana wanadamu tumeumbiwa kuabudu ili tujihisi tuko salama katika eneo la kiroho maana pasipo kuamini maisha yanakosa radha sahihi kwa kujihisi tuna upungufu maeneo eneo,
Lakini nakushauli ndugu yangu weka IMANI yako katika neno la MUNGU, maana neno la MUNGU ni taa yetu huangaza maisha yetu na kutufanya tuwe salama katika maisha yetu,
Kuwa salama kunategea umechagua kuishi maisha ya namna gani hapa duniani yaani umechagua kusimamia imani ipi katika MUNGU wa kweli au mungu wa uongo ambae ni shetani,
Usiogope MUNGU yupo upande wetu sisi tulioweka tumaini letu kwa kwake na ameahidi kutotuacha kamwe hata ukamilifu wa ulimwengu yeye atakuwa pamoja nasi daima Usiogope unamwamini MUNGU muamini na mwana yaani YESU KRISTO,
Alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu yohana 3:16-17 inasema kwa maana Jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili kila aaminie asipotee bali awe na uzima wa milele, asie mwamini amekwisha hukumiwa.
Hatupaswi kugopa kwa kuwa MUNGU alimtoa mwanae wa pekee ili sisi tuwe na UJASIRI hivyo Hatupaswi kuogopa na kupitia damu yake YESU msalabani tunahesbiwa hali kwayo, ndugu yangu mpendwa msafiri mwenzangu andaa maisha yako sasa maana baada ya kifo ni hukumu kama bado hujampa YESU maisha huu ni wakati sahihi kwako kumpa YESU maisha yako yaani kumpokea awe BWANA na MWOKOZI wako,
Usiogope watu wanaokuzunguka wewe mtazame yeye awezae kukupa maisha mapya yasio na machozi maisha yenye mafanikio na furaha isiyo na majuto.
Comments
Post a Comment