MLEE MTOTO KATIKA NJIA IMPASAYO ILI AKUE KATIKA IMAN YA KIKRISTO
Waamuzi 2:8-11
•Kisha Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, akafa, naye alipata umri wa miaka mia na kumi.
•Nao wakamzika katika mpaka wa urithi wake katika Timnath-heresi, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, upande wa kaskazini wa mlima wa Gaashi.
•Tena watu wote wa kizazi hicho nao walikusanywa waende kwa baba zao; kikainuka kizazi kingine nyuma yao, ambacho hakikumjua Bwana, wala hawakuijua hiyo kazi ambayo alikuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.
•Wana wa Israeli walifanya yaliyokuwa ni maovu mbele za macho ya Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.
Watoto wako usipowafundisha habari za Mungu shetan atawafundisha na atapandikiza vyakwake badae aje akusumbue, ndipo utukutu, ukorofi na kiburi vitakapojaa kwa mtoto wako,
Watoto nikama karatasi nyeupe unatakiwa uijaze kwa kuandika sasa ikiwa mtoto wako hutakua unamsisitiza kwenye Neno la Mungu na mwenendo mwema hataweza kuenenda kama Mungu anavyotaka,
Kuna mambo amabayo tunawaachilia watoto ambayo nihatari sana wanafikia hatua ya kuwa watu wazima wanaharibika kwakua hawakuambiwa baadhi ya vitu wakati wa makuzi yao,
Amri 10 za Mungu,
Ukisimama na kumwambia madhara ya amri kumi na ukimuombea ulinzi wa Mungu juu ya akili na ufahamu wake anajengeka na kuikataa dhambi kwakua Mungu anapata nguvu kwakua Neno lake linajaa kichwani.
Heshima, utii kwa watu wote. Amri ya nne
Watoto na vijana wamekua hawana tabia njema kwa watu wazima sababu hawajasimamiwa kwa bidii juu ya heshima, Wakristo sisi ndio wakuwafundisha mambo mazuri watoto wetu ili kujenga jamii Yenye busara na baraka lkn cha kushangaza baadhi ya wakristo hawana muda na watoto wao kila siku wako bize na maisha na kusahau majukumu yao ya kifamilia,
MAVAZI
Hiki ni kitu kikubwa sana kwa watoto kwakua kuna maroho machafu yanayowavamia watoto kutokana na mavazi, kuna mapandikizi Mengi ndio maana maroho ya uchungu, kukataliwa, ushoga na umalaya vinawavaa na kuwafunga,Mvalishe mtoto mavazi ya staha, ya heshima, ukimvalisha mavazi mabaya hukumu itakua juu yako kwakua umemfundisha mwenendo wa umataifa,
Usikae kimya ukiona anaanza kutoka nje ya mstari piga kelele na Muelekeze madhara ya hayo mambo,
Wewe yamkini ungeachiliwa ulipokua mtoto na kua hivyo sababu wazazi wako hawakusimama katika kukwambia visivyofaa, hawakuweka mkazo ulipotoka nje ya mstari, hawakuwa wamesimama kwenye Neno ili kukujulisha kikupasacho kufanya.
Misingi imeharibika sasa niwewe wa kumfundisha mtoto wako maadili mema ili aje kujenga jamii yenye maadili iliyo na kibali mbele za Mungu,
EPUKA
Kumvalisha mtoto visuruali, vimini, na nguo zinazoonyesha mpaka ndani (Transparency) na vikaptula kwa binti, kwa wakiume usimvalishe mafurana yenye mapicha ya watu mashuhuri wakimataifa kwakua hujui hao watu walikua wanatumia nguvu gani endapo watavaa hayo maroho yatawashikilia na kuwasukuma kufanya mambo mabaya,Usiwavalishe watoto suluali zilizochanika chanika kwakua kuna roho zitawafuatilia ndipo badae atakua si msikivu na mwenye tabia chafu
Ukichanganya na Ibada za kila siku nyumban mtoto atajengeka hofu ya KiMungu ndani yake,
IBADA ZA NYUMBANI
Niseme kidogo kuhusu ibada za nyumbaniIbada za nyumbani ni za muhimu sana katika kumlea mtoto na kumfundisha maadili stahiki na kumjengea kumjua MUNGU kumbuka nimesema mtoto ni kama karatasi nyeupe hivyo mfanyapo ibada nyumbani mnaandika maneno ya Mungu ndani yake na ndio maana Biblia inasema mlee mtoto katika njia sahihi hata atakapo kuwa hataicha.
Kutowafundisha ukuu na uweza wa Mungu kwa watoto na vijana wa israel ilipelekea watoto kutokumjua Mungu wala kutokujua sababu ya ukombozi wao,
mtoto wako nimuhimu sana kumfundisha mambo ya KiMungu ili ajae uchaji wa ki-Mungu ndani yake,
Mpe nafasi ya kutafari na kufundisha hapo nyumbani, mpe nafasi ya kuomba na kuimba ili kichwani ajengeke vyaki-Mungu, ukimzoesha hivyo ndipo utumishi utakapoumbika na Kristo kutawala katika nyumba yako na jamii yako
Ila hayo yawe ni yamwendelezo isiwe kwa muda mfupi akikua akue nayo ndipo utakapo mshangilia Bwana kwa kumponya mtoto wako na mabaya ya ulimwengu
JAMII YAKO
Niwewe ndie wakujenga jamii yenye maadili utakuja kudaiwa na Mungu kwakua hukuusambaza ufalme wake wala kukemea maovu badilika leo.
Tubu kwaajili ya watoto wako kwa yale waliorithi toka kwenu wazazi na mabibi zao, vunja maroho yote na weka mpaka wa damu juu ya laana na maagano yote, mwambie Bwana afundishe watoto wako, mwambie Roho mtakatifu akupe maalifa na ufahamu wa kumfundisha mtoto wako.
Nakutakia baraka za Bwana katika jina LA Yesu.
usisahau kushare ujumbe huu muhimu kwa jamii yetu.
Kwa mawasiliano zaidi usisite kuwasiliana nasi kwa simu number +255756717689 au email
makubimsafiri@gmail.com
Comments
Post a Comment