NAMNA YA KUPATA MAJIBU YA NDOTO/MAONO


1. Mara tu, baada ya maono au ndoto kuisha, muda ule ule, unapaswa kutulia kimya na kutafakairi kwa muda, na hapo ndipo roho wa Mungu anapoweza kutupa maelezo ya maono/ndoto hiyo (Matendo 10:9-20).

Izingatiwe kuwa si lazima Mungu afanye hivyo kwa muda huo, hivyo endapo hatafanya hivyo, ni vema sasa ufuate hatua ya pili ambayo ni hii ifuatayo.

2. Kumwomba Mungu tafsiri moja kwa moja.
Baada ya kutulia kwa muda,kama hujapata tafsiri, tunapaswa kumwomba Mungu mwenyewe atafsiri (Daniel 2:16-19). Na endapo hatujapata majibu bado, tunapaswa kulala na hata kuisahau ndoto hiyo,hapo Mungu huweza kukuletea ndoto ile ile tena huku akiifafanua kwa namna flani.

Anaweza kuleta moja au hata zaidi. Tunapaswa kuwa na subira pia (Mwanzo 41:17-23) kwani pengine, anawezaa kukukumbusha juu ya matukio utakayo yaona katika maisha yako siku zitakazofuata. (Waamuzi 7:7-15)

3. Kuuliza Katika Maono au Ndoto.
Hatua hii, hutumika mara unapokuwa unapewa maono moja kwa moja kutoka kwa wale watu au viumbe wanaokuwa wanakupa ujumbe huo. Mara zote, kiumbe yeyote atakaye kuja kwako, atajitambulisha kuwa yeye ni nani na ametumwa na nani kwako, kisha ndiyo atatoa ujumbe aliotumwa kwako.

Kama ni malaika wa Mungu, kwanza atakusalimia kwa salamu ya Usiogope na hapa utajisikia amani sana moyoni mwako (Daniel 10 :19, Luka 1 :13, 30) na endapo utaendela kuogopa kemea kwa jina la Yesu, huyo hatakuwa Malaika. Matokeo ya kukemea yatakuthihirishia kuwa huyo ni nani.

Angalizo ; malaika yeyote atakayetumwa kwako atakapojitambulisha, atakachokwambia utapaswa kukipima kulingana na neno la Mungu.

Comments

  1. Maono au ndoto watu wengi wamekuwa wakichukulia kuwa ni kitu Cha kawaida au kimetokea kwa kwa bahati mbaya au nzuli lkn hakuna kitu ktk maisha ya mwanadamu kinakuja bila ya kuwa sababu au maana ktk maisha yako ya siku zijazo hivyo ni vyema kuwa makini tuoyapo ndoto au tuonapo maono na ni kwa majibu wa Biblia kwamba siku za BWANA atamimina ROHO yake ulimwenguni vijana wataona maono na wazee wataota ndoto lkn haimaanishi kwa vijana hawawezi kuota ndoto au wazee hawawezi kuona maono hivyo nikuombe ndugu yangu usizalau maona au ndoto huwa yanabeba ujumbe muhimu sana kwa ajili ya future yako.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

NINI MAANA YA NAFSI, ROHO, MOYO NA MWILI.?

USHUHUDA WA ALIEKUWA WAKALA WA SHETANI

BWANA YU PAMOJA NAWE EE SHUJAA