NINI MAANA YA NAFSI, ROHO, MOYO NA MWILI.?
NINI MAANA YA NAFSI, ROHO, MOYO NA MWILI.? 1. ROHO Neno “ roho ” asili yake ni katika lugha ya Kiyunani likiitwa “ Pneuma” ambalo maana yake kwa kiswahili ni “ pumzi” . Pumzi ya namna hii ni pumzi iletayo uzima yaani mtu anakuwa hai. Bila roho hakuna mtu anaweza kuwa hai 2. NAFSI Neno “ nafsi ” ni sehemu ya mwanadamu inayohifadhi akili na hisia. Hivyo kusema nafsi ya mwanadamu ni sawa na kusema akili,ufahamu na hisia zinakokaa. 3. MOYO Moyo ni sehemu ya kiroho ya mwanadamu ambako hisia za mwanadamu na matamanio ya mwanadamu hukaa. 4.MWILI Mwili ni gamba la nje linaloibeba roho Kwa lugha nyingine mwili ni nyumba ya kuishi roho. N.b Katika baadhi ya maandiko kwenye Biblia yanazungumza moyo yakiwa na maana ya nafsi na pengine yanazungumza nafsi yakiwa na maana pia ya moyo wa Mtu. Kwa sababu nafsi na moyo ni kama kitu kimoja. MUNGU akubariki. Mt Daudi Makubi Mtenda Kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO ...
Comments
Post a Comment