KIZAZI CHA WAKRISTO VIJANA


KIZAZI CHA WAKRISTO VIJANA:

1.Daima tuko sawa na hatukubali kabisa kuonywa, kukemewa na kukaripiwa. Atuonyaye, kutukemea na kutukaripia anasomeka kama adui wa kumwepuka kwa gharama zote tena akizidi kutufuata fuata tunamwambia achana na maisha yangu, hayo ni yangu hayakuhusu wewe.

2. Tunapenda kuimba kanisani lakini hatusomi bibilia zetu nyumbani wala kuomba.

3. Tumejaa tamaa, hamu ya kufanya ngono na hisia ambazo sisi tunaziita upendo au mapenzi.

4. Tunataka tuwe na ndoa bora, lakini tunapokuwa tumefika umri wa miaka 25 tunakuwa tulishakuwa ndani ya mahusiano ya kimapenzi kwa miaka kumi tayari. Wakati mwingine tumeshakuwa na wapenzi wa kike na wa kiume hata kuliko wazazi wetu.

5. Ngono na matendo machafu ya kingono sasa ni sehemu ya mahusiano yetu na tunaiita Mahaba/Mapenzi.

6. Tunataka kuwa matajiri maishani, wakati huo huo tunatumia fedha zetu zote kununua simu za kisasa kama iphone, samsung galaxy, htc, Blackberry, vifaa vya mawasiliano vingine kama ipad, tablets, laptops na camera za kisasa ambazo tunashindwa hata kutumia zaidi ya asilimia sabini ya vitu vilivyomo.

7. Hatulipi zaka zetu wala kutoa sadaka tukisingizia sisi ni wanafunzi.

8. Tunajiita wanawake wa kikristo lakini tunavaa kama waigizaji wa sinema, nusu uchi kama sio uchi kabisa alafu tunasema ndo mitindo ya mavazi ya kisasa bila kujali kama ushuhuda wetu na ukristo wetu unaathiriwaje.

9. Tunapenda anasa kuliko kumpenda Mungu.

10. Kanisani utatuona tukiwa tumeinua mikono huku twaimba nyimbo za taratibu kama tunaabudu vile lakini kwenye simu zetu mifukoni mwetu kuna picha za wanawake waliyo nusu uchi na wengine uchi kabisa, nyimbo za muziki wa kizazi kipya, maisha ya kujirusha na kutumia na tuna namna nzuri ya kulielezea hilo na kulifaulisha.

11. Tunaishi maisha ya huku na huku na mtu asikuulize utasikia achana na kufuatilia maisha yangu.

12. Tukienda kanisani wala neno halituhukumu tena kwa habari ya maisha tunayoyaishi maana mioyo imefanywa migumu na udanganyifu wa dhambi na tuna kiburi kuliko Lewiathani.

Mungu aliyaona haya akatuonya kwenye:

II Tim. 3: 1 - 6.

1 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. 2Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, 3wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, 4wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; 5wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao. 6Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;

Kijana hizi ni nyakati za hatari kuliko ambavyo upo tayari kukubali.
BADILIKA !
TUBU !
AMA SIVYO HUKUMU YA MUNGU NI FUNGU LAKO !!!
 HUTAKWEPA.√

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

NINI MAANA YA NAFSI, ROHO, MOYO NA MWILI.?

USHUHUDA WA ALIEKUWA WAKALA WA SHETANI

BWANA YU PAMOJA NAWE EE SHUJAA