AINA ZA HASIRA ZA WANAWAKE NA HEKIMA YA MKE KWA MUMEWE.
AINA ZA HASIRA ZA WANAWAKE NA HEKIMA YA MKE KWA MUMEWE. 1. Kuna mwanamke ambaye akikasirika, huishia kulia tuu! 2. Lakini mwingine akichukia, anaongea saanaa muda wote hadi ikukere! 3. Mwanamke mwingine akikasirika, ananuna, haongei! Mtapishana tu kimya kimya. Mawasiliano kibubu-bubu. Shavu limejaa kama Kobra! 4. Mwingine akishikwa na hasira, period ya ghafla ghafla inafuata! 5. Wako wanawake ambao, akichukia, Atakachokishika usipokimbia anakutandika na anaweza kukuchoma na kisu,, majuto baadaye! 6. Mwanamke mwingine akikasirika, hasira zake zinaishia kwenye kuvunja-vunja vyombo. Au saa nyingine kugombeza- gombeza wafanyakazi na watoto! Dizaini hii, huwa ni wale waliokosa kukidhiwa haja za kihisia/ ndoa na waume zao! 7. Mwanamke mwingine akikasirika, Mtajuana kitandani panapo usiku, Nakwambia utaungama yoote! 8. Kuna wengine wakitibuliwa, hukimbilia kufunga mabegi na kuondoka! 9. Wapo ambao wakikasirika, wanagoma kupika! 10. Wengine wakichukia, wanaam...