BIBI AELEZA SIRI TISA ZA KUISHI MIAKA 100 MIA MOJA
Vitabu vya dini vinaeleza miaka ya mwanadamu kuishi ni 70 na ukiwa na nguvu ni miaka 80, lakini si kwa Bi Illuminata Mosha ambaye amevuka umri huo na mwezi ujao atagonga miaka 101.
Ni mzee ambaye bado anajikongoja kufanya shughuli za kila siku nyumbani kama kuhudumia mifugo iliyo katika banda la mbao lililojengwa pembeni mwa nyumba yao ya tofali za saruji, milango na madirisha ya nondo.
Kwa kumuangalia, bibi huyo hatofautiani na wazee wengine wenye umbile kama lake, lakini anapokwambia umri wake, ndipo unaona tofauti.
Moyoni mwake ana siri sita kubwa zilizomuwezesha yeye na watu waliokua naye, kuishi miaka mingi na bila ya kusumbuliwa na matatizo.
“Tangu tukiwa wadogo tulikuwa tunakula vyakula vya asili,”
Anasema kikongwe huyo anayeonekana kuwa na ufahamu mkubwa wa masuala ya afya na kijamii wakati alipoongea nyumbani kwake Kata ya Kilema wilayani Moshi.
Bibi huyo anataja vyakula vya asili, kutotumia mafuta ya viwandani, kula nyama na maziwa, kutumia dawa za asili, kuwa na usiri na kuwa na upendo kuwa ni mambo yaliyowafanya wasipatwe na magonjwa yanayoua mapema vijana wengi kwa sasa kama shinikizo la damu, saratani na Ukimwi.
Anasema utaratibu wa ulaji wa sasa unaotumia vyakula vya viwandani, ndiyo unaochochea kizazi cha sasa kuandamwa na magonjwa na hata kufariki dunia mapema.
“Sisi zamani tulikuwa tunakula vyakula vya asili kama maharage yanayosongwa kwa kuchanganywa na ndizi, viazi vikuu. Tulikuwa tunakula nyama kwa wingi na maziwa ya kutosha,” anasema baada ya kuulizwa siri ya kuishi maisha marefu.
“Ili ule nyama vizuri, ulitakiwa kula dawa ya asili ya kusafisha tumbo ndio ule nyama hiyo na tulikuwa tunafuga ng’ombe kwa wingi hivyo tulikuwa tukipata kwa wingi nyama na maziwa.
“Hivi vyakula vya kisasa tulikuwa hatuli kabisa.”
Anasema hata mafuta ya kupikia, walikuwa wakitumia ya asili yanayotokana na wanyama kama samli.
“Maradhi kama shinikizo la damu, kisukari, saratani yalikuwa hayapo kabisa ndio maana tumeweza kuishi maisha marefu,” alisema.
“Kwa mfano hivi sasa mimi sili chakula chenye mafuta wala chumvi maana najua nikiepuka vyote hivyo sitasumbuliwa na shinikizo la damu ambao unatesa hadi watoto wadogo.”
Upendo huongeza siku
Bibi Illuminata pia anasema upendo ni muhimu kumuwezesha mtu kuishi maisha mazuri.
Anasema enzi zao walipendana na kusaidiana katika matatizo, tofauti na wakati huu ambao mtu husumbuka na tatizo lake mwenyewe.
“Ukipata tatizo kwenye familia, ni lako mwenyewe kwa hiyo unabebana nalo hadi unadondoka kwa presha,”
Anasema.
“Sisi tulikuwa na mshikamano wa ukweli, upendo wa ukweli na undugu wa ukweli. Hivyo tulikuwa tukibebana kwenye matatizo. Ilikua si rahisi mtu kupata msongo wa mawazo.
“Watu wa sasa wamebadilika. Unaweza kuwa na tatizo ukamshirikisha mwenzako badala ya kukusaidia anafanya matangazo. Hivyo kwa sasa mtu anaona ni heri akae na tatizo lake.”
Matumizi ya dawa za uzazi
Katika mazungumzo yake bi Illuminata ambaye pamoja na wenzake wengi wa enzi hizo aliishia darasa la nne, pia aligusia suala la matibabu na uzazi wa mpango.
“Dawa za hospitali zinakuwa na kemikali nyingi ambazo japo zinasaidia, huchangia kufupisha maisha,” anasema.
“Mfano zamani tulikuwa hatutumii dawa za uzazi wa mpango kama ilivyo sasa. Hata haya magonjwa yaliyopo sasa ya wanawake wengi kuwa na uvimbe kwenye uzazi, yanatokana na madawa haya.
“Sisi tuiishi kwa kutumia miti shamba ndio maana hadi sasa tunaishi bila kusumbuliwa na maradhi sana. Kwa sasa wazee wa miaka mingi iliyopita tunasumbuliwa na magonjwa ya uzee tu.
Anasema hata suala la kujamiiana lilifanywa kisiri, licha ya kuwa walikuwa wakiishi kwenye maboma yao tofauti na nyumba za waume wao ambazo zilikuwa zikiheshimika.
“Kama mtu akimtaka mwenzake (tendo la ndoa), tulikuwa tukikutana kisiri kabisa na hamna mtu yeyote aliyekuwa akijua maana tendo la ndoa lilikuwa likiheshimika sana,”
Anasema.
“Ni tofauti na sasa watu wamekuwa na utamaduni mbovu. Vijana wetu sasa wamekuwa hawatulii na ndoa zao, ndio maana ndoa nyingi zinavunjika.”
Hakuna talaka
Kuhusu maisha ya ndoa, bibi huyo alisema kulikuwa hakuna talaka na kama kukitokea kutoelewana, suala hilo lilisuluhishwa.
“Ndio maana sisi tuliweza kudumu kwenye ndoa zetu. Tuliwaheshimu sana waume zetu, hata kama tulitofautiana kidogo,” anasema.
“Ilikuwa si rahisi watu kugombana hadi kupeana talaka na kama kulitokea tatizo kama hilo ukoo unakaa na kusawazisha jambo hilo na mambo mengine yalikuwa yakiendelea bila tatizo lolote.
“Lakini sasa hivi kinachomaliza vijana wa leo ni huu utandawazi watu wanaiga tamaduni za nje.”
Bibi huyo alisema vijana wengi wa sasa wanafariki wakiwa na umri mdogo kutokana na kuendekeza mambo ya ngono, wengi wao sasa hivi wanakufa kwa ugonjwa wa Ukimwi.
Bibi Illuminata anaeishi Mtaa wa Kilema, Moshi Vijijini na kwa sasa hujishughulisha zaidi na kukatia mifugo chakula kutoka shamba lao lililo jirani na nyumba yao.
Pia, bibi huyo, ambaye hakuwahi kuajiriwa tangu alipomaliza darasa la nne, hujishughulisha na kulima bustani iliyo pembeni ya nyumba aliyojengewa na watoto wake, akiishi na wajukuuu wake.
Kumbe katika maisha siri kubwa hapa ni UPENDO
Upendo haubagui
Upendo hauhesabu mabaya
Upendo huvumilia
Upendo huongeza siku
Upendo hudumisha amani
Upendo Upendo Upendo ndio Furaha na nguzo imara ya maisha ya mwanadamu awaye yoyote hapa duniani,
Ni vyema tukatambua kuwa Pendo halisi asili yake ni MUNGU.
Tunapotambua ivyo basi tutapenda na kupendana sawa sawa na Mungu atakavyo Mungu (sawa na mapenzi yake MUNGU)
Wanadamu wengi wamekuwa na Upendo ambao ni wa msimu, anakupenda leo kwa sababu anatarajia kitu sio bure bure,
Embu tuangalie Maandiko Kidogo
Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu.
8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
1Yohana 4;7,8
PENDO LETU likisukumwa na MUNGU mwenyewe hakika litazaa matunda, maana litakuwa la kila iitwapo leo, sio leo Upendo, kesho CHUKI,
APENDAYE AMJUA MUNGU,AMBAYE HAKUPENDA HAKUMJUA MUNGU.
Ni wakati wa kujitafakari na kuona ni aina gani ya Upendo iko ndani yetu.
Tuishi Vile Kristo anataka,UPENDO wa KRISTO ni wa milele, hauchuji,haujengwi na vitu au matukio,bali wajengwa na nguvu za Mungu zilizomo ndani yetu.
MUNGU AZIDI KUKUBARIKI UNAPOTAFAKARI UPENDO WA MUNGU KWAKO, NA UPENDO WAKO KWA WENGINE.
Mt Daudi Makubi
makubimsafiri@gmail.com
Share na wengine, Mungu akubariki
MORE BLESSINGS ARE AHED OF YOU

Comments
Post a Comment