INAWEZEKANA KABISA MWANAUME KUWA NA MWANAMKE MMOJA
INAWEZEKANA KABISA MWANAUME KUWA NA MWANAMKE MMOJA Yaani sisi ni tai, ila hatuelewi, tunajifahamu kama kuku. Kwamba tunao uwezo mkubwa wa kuwa mwanaume wa mwanamke mmoja lakini tumeaminishwa kinyume chake tumeamini na tunaishi ndani ya uongo huo uliopikwa vizuri. Mkulima mmoja aliokota yai la ndege tai akalichukua na kwenda kulichanganya na mayai ya kuku wake aliyekuwa anatamia. Baada ya muda kuku akatotoa pamoja na lile yai la tai. Mama ambae ni kuku akamlea tai akijua ni mtoto wake, Tai akakua pamoja na vifaranga vya kuku, Akachakura jalala moja akitafuta chakula kama vifaranga wengine, Akienda huku, ‘kampani’ yake ilikuwa ni kuku, akirudi huku ‘kampani’ yake ilikuwa ni kuku. Siku moja, akiwa na kuku wengine akaona familia ya tai inapaa angani. Akatamani kuwa mmoja wa wale tai, kuwa kule juu, mawinguni akamgeukia kuku mmoja aliyekuwa karibu yake, akamwambia. “Natamani ningekuwa tai.” “Haitawezekana.” Kuku akamjibu, kisha akaongeza. “Wewe umeumbwa kuku, na utabaki kuwa ku...