KUNA GHARAMA YA KULIPA ILI UTEMBEE NA MUNGU
KUNA GHARAMA YA KULIPA ILI UTEMBEE NA MUNGU 🔹Watu wengi sana wanapenda kutembea na Mungu katika maisha yao, na hicho ni kitu kizuri sana, lakini ni watu wachache sana ambao wanaelewa gharama wanayotakiwa kulipa ili wafanikiwe katika jambo hilo. 🔸Mungu anapenda kuona watu wake wanatembea pamoja nae kama walivyofanya wakina Henoko, Ibrahimu, Daudi n.k, lakini ana kanuni zake ambazo watu wake wanatakiwa kutembea nazo kila wakati. 🔹Kanuni kubwa ni kufanya mapenzi ya yake (yaani mapenzi ya Mungu) katika maisha yako. Yohana 8:28-29. 28. Basi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo. 29. Naye aliyenipeleka yu pamoja nami, hakuniacha peke yangu; kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo. 🔹Unapotaka kufanya mapenzi ya Mungu na kutembea pamoja nae katika maisha yako, unatakiwa kufahamu na kuzingatia mambo yafuatayo; 1. LA...