MAARAFA NI NINI?
Watu wengi wanasema unaangamia kwa kukosa maarifa lakini hawajui maana ya maarifa nini. Maarifa ni nini? Maarifa ni njia inayotumiwa kujitoa katika shida. Maarifa ni njia ya kupata kitu. Maarifa ni Elimu au ujuzi. Biblia inazungumza hapo juu kwamba watu wengi wanaangamizwa kwa kukosa maarifa, maarifa yanayozungumzwa hapa ni elimu na ujuzi sahihi wa Neno la MUNGU. Maana ya kwanza ya maarifa ni njia inayotumiwa kujitoa katika shida. Shetani ameleta shida nyingi sana na vifungo vingi sana kupitia mawakala zake wachawi, waganga na mizimu na watu wengi sana wameangamia kwa sababu tu wamekosa maarifa ya kuwatoa katika shida hizo. Biblia inajulisha ikisema kwamba Kumcha MUNGU ndio chanzo cha maarifa sahihi yanayoweza kumsaidia mtu ili atoke katika shida mbalimbali za kiroho, Hiyo iko Mithali 1:7 '' Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.'' Biblia inasema Ni wajinga peke yao ndio wanaoweza wakadharau Neno la MUNGU la kuwapa maarifa sahihi ...